Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza uchunguzi ufanyike kwenye ujenzi
wa madarasa na mabweni ya Shule ya Wasichana Nangwa wilayani Hanang’,
Manyara kutokana na madai ya kuwapo kwa ubadhirifu wa Sh807 milioni
unaodaiwa kufanywa na maofisa wa Wizara ya Elimu.
Samia
alisema hayo jana baada ya kuweka jiwe la msingi la bweni la wasichana
wa shule hiyo lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 160 lililojengwa na
halmashauri ya wilaya hiyo kwa Sh150 milioni.
Alitoa
agizo hilo baada ya mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kusema
baadhi ya maofisa wa Wizara ya Elimu wanafanya ufisadi kwa kufuja fedha
za ujenzi wa madarasa na mabweni ya shule hiyo.
Alisema
maofisa hao wametumia zaidi ya Sh807 milioni kujenga madarasa na
mabweni wakati bweni lingine kubwa zaidi limejengwa na halmashauri kwa
Sh150 milioni.
“Mheshimiwa
Makamu wa Rais, nataka nikuhakikishie mkoa huu siyo wa majaribio wa
watu kufuja fedha kwani nikiwaandikia barua wanipe taarifa wanadai jengo
linajengwa na wizara siyo mkoa,” alisema Mnyeti.
“Kwenye
Mkoa wa Manyara miradi inasimamiwa kwa ubora ndiyo sababu mwaka huu
tukashika nafasi ya pili kitaifa kwenye mbio za Mwenge kwa ubora wa
miradi.”
Aliwapongeza
mkuu wa Wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti na mkurugenzi mtendaji
Bryceson Kibassa kwa kusimamia maendeleo. “Hawa ni wasaidizi wangu
wazuri wanaotimiza wajibu wao ipasavyo,” alisema Mnyeti.
Mama
Samia ambaye yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi, aliagiza
uchunguzi ufanyike mara moja ili kubaini namna ya fedha hizo
zilivyotumika katika ujenzi huo.
“Kama
jengo la bweni kubwa la halmashauri limetumia fedha kidogo na lina
ubora inakuwaje huku wametumia fedha nyingi namna hivyo? Ni lazima hilo
lichunguzwe,” alisema.
Pia,
aliridhia bweni lililojengwa na halmshauri hiyo aliloweka jiwe la
msingi kuitwa jina lake kisha akaendesha harambee ya kusaidia shule hiyo
na kupatikana Sh20 milioni.
No comments:
Post a Comment