Benki
Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa usimamizi wa Bank M Tanzania Plc
(Bank M) kwa siku 60 zaidi kuanzia tarehe 2 Novemba 2018.
Kwa
mamlaka iliyopewa chini ya kifungu namba 56 (1) (g) (iii) cha Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania
ilichukua usimamizi wa Bank M kuanzia tarehe 2 Agosti 2018 baada ya
kubaini kuwa benki hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na
matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni
zake.
Baada
ya kuchukua usimamizi, Benki Kuu ya Tanzania ilisitisha shughuli za
utoaji wa huduma za kibenki za Bank M kwa muda wa siku tisini (90) ili
kuipa nafasi Benki Kuu ya Tanzania kutathmini hatua za kuchukua ili
kupata ufumbuzi wa suala hilo.
“Benki
Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini
hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M
haujakamilika; hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku
60 kuanzia tarehe 2 Novemba 2018,” kwa mujibu wa taarifa kwa umma
iliyotolewa leo.
Aidha,
Benki Kuu ya Tanzania inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda
maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu
katika sekta ya fedha.
No comments:
Post a Comment