Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo
yamesema Bungeni jana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula
Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.
“Katika
kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa
ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro,
Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero,
Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti,
Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga” amefafanua Naibu Waziri Mabula.
Mabula
anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278
Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni
ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781
milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.
Aidha
anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo,
Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya
Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya
ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na
ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Mbali
na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba
yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa
Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya
Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.
No comments:
Post a Comment