WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela orodha ya matrafiki wanaodaiwa kuwaomba rushwa madereva wa noah wilayani Lushoto.
Majina
ya trafiki hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa madereva wa noah wanaofanya
kazi ya kusafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo yaliwasilishwa kwa
Waziri Mkuu kupitia mabango.
Waziri
Mkuu alimkabidhi majina hayo jana jioni (Jumatano, Oktoba 31, 2018)
baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa
Sabasaba, Lushoto mjini.
Baada
ya kumkabidhi majina hayo alimuagiza afanye uchunguzi wa tuhuma za
rushwa zinazowakabili askari hao na kisha awasilishe taarifa kwake leo
Alhamisi Novemba 1, 2018.
Mbali
ya wananchi kuwasilisha malalamiko hayo, Pia mbunge wa Lushoto, Shaaban
Shekilindi alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo
inayowakabili wananchi.
Awali,
Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya
Lushoto katika ukumbi wa chuo cha Mahakama Lushoto ambapo aliwasisitiza
wafanye kazi kwa bidii.
Alisema
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haina
msamaha na mtumishi wa umma asiyetaka kufanya kazi kwa bidii na
kuzingatia weledi.
Alisema
watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya
utumishi ili waweze kutimiza lengo la Serikali la kuwahudumia wananchi
kwa kutumia taaluma zao.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani
Tanga alisema Serikali haina msamaha na mtumishi asietaka kubadilika na
kufanya kazi.
Pia,
Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma wahakikishe fedha zinazotolewa
na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka Wakuu wa Idara kutumia kitabu cha ilani ya
uchaguzi cha CCM cha mwaka 2015/2020 kwa sababu kina maelekezo
wanayopaswa kuyatekeleza.
“Kitabu
kile kina maelezo ya msingi yaliyotolewa na Rais. Dkt. Magufuli ambayo
yanatakiwa yapewe kipaumbele cha utekelezwaji, wakuu wa Idara ni muhimu
musome na kutekeleza.”
Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa wilaya wahakikishe
wanasimamia utekelezwaji wa maelekezo yote yaliyoainishwa kwenye kitabu
cha Ilani katika maeneo yao.
Kuhusu
changamoto ya upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali nchini, Waziri
Mkuu alisema Serikali inatambua na kwamba suala hilo linaendelea
kufanyiwa kazi.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba na kuwapongeza wakazi hao
kwa kutunza misitu.
Alisema
maeneo mengi nchini wananchi wamekata miti na kusababisha kukauka kwa
vyanzo vya maji, ambapo ni tofauti na wilaya ya Lushoto ambayo bado ina
misitu minene.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wote wa vijiji na kata
waainishe sehemu zote zenye misitu na vyanzo vya maji katika maeneo yao
na wahakikishe wanayalinda.
Alisema
mtu yeyote atakayebainika kuharibu mazingira hayo iwe kwa kuchoma au
kukata miti achukulie hatua kali. “Ni marufuku mtu yeyote kukata miti
bila kibali cha Serikali.”
Nae,
Mbunge wa Lushoto Shekilindi alimuomba Waziri Mkuu awasaidie katika
kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa katika
jimbo hilo ikiwemo ya afya.
Mbunge alisema kwa sasa hospitali ya wilaya hiyo inakabiliwa na ukosefu wa mashine ya x
rey, hivyo kusababisha wananchi kusafiri hadi Korogwe au Tanga kufuata huduama hiyo.
Waziri
Mkuu alisema tayari ameshamuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupeleka mashine ya x-rey katika
hospitali hiyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, NOVEMBA 1, 2018.
No comments:
Post a Comment