Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni limefanya upekuzi nyumbani kwa Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.
Jebra
 Kambole, wakili wa mbunge huyo wa Kigoma Mjini amesema kuwa upekuzi huo
 umefanyika Masaki jijini hapa, nyumbani kwa mbunge huyo.
Jana 
 asubuhi Zitto alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake na kupeleka 
katika Kituo cha polisi Oysterbay ambako alihojiwa kwa saa tatu na 
kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi.
Kambole
 amesema baada ya mteja wake kupelekwa kituo kikuu cha polisi, hakulala 
hapo alihamishiwa kituo kingine kilichopo Mburahati ambako aliondolewa 
leo asubuhi na kurudishwa kituo cha polisi Oysterbay.
“Leo
 asubuhi mteja wangu aliongozana na polisi hadi nyumbani kwake Masaki 
kwa ajili ya kufanya upekuzi kisha akarudishwa kwenye kituo cha 
Oysterbay,” amesema.






No comments:
Post a Comment