Marekani imetangaza kuwa leo Nov 5 imeirejeshea vikwazo nchi ya Iran vitakavyolenga sekta ya mafuta na sekta ya kifedha.
Marekani imesema imeiwekea Iran vikwazo vigumu zaidi ambavyo haijawahi kuiwekea. Vikwazo hivyo vitalenga mauzo ya mafuta, usafiri kwa njia ya baharini na mabenki ambavyo vyote ni muhimu sana kwa uchumi.
Maelfu
ya raia wa Iran wakiwa na mabango yaliyoandikwa "Kifo kwa Marekani"
wameandamana wakiitaka serikali yao kutofanya mazungumzo yoyote na
Marekani.
Jeshi la Iran nalo limesema kuwa litafanya mazoezi ya kijeshi leo Jumatatu na Jumanne kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.
Marekani
imetangaza vikwazo hivyo baada ya Rais Trump kutangaza kujitoa
kwenye mkataba wa mwaka 2015 uliolenga kupunguza mipango ya nyuklia ya
Iran.
Marekani
inasema inataka kuzima vitendo viovu vya Ina vikiwemo udukuzi wa
mitandao, majaribio ya makombora ya masafa marefu na uungaji mkono wa
makundi ya kigaidi mashariki ya kati.
Zaidi
ya watu 700, kampuni, vyombo vya habari na ndege kwa sasa vimewekewa
vikwazo, yakiwemo mabenki makubwa, wauza mafuta na kampuni za usafiri wa
baharini.
Wakati
hayo yakijiri, Uingereza , Ujerumani na Ufaransa ambazo ni kati ya nchi
zilizo kwenye makubaliano ya nyuklia zote zimekataa vikwazo hivyo vya
Marekani dhidi ya Irani.
Zimeahidi
kuzisaidia kampuni za Ulaya zinazofanya baishara halali na Iran na
kubuni njia mbadala za malipo ambazo zitasaidia kampuni kufanya bishara
bila ya vikwazo vya Marekani
No comments:
Post a Comment