Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku kumi nne zaidi (14) kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 zilizokaguliwa kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao.
Tamko
 hilo limetolewa jana jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya 
Jamii Dkt. John Jingu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari 
kuhusu utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa kwa Mashirika 
Yasiyo ya Kiserikali.
Ufafanuzi
 ulitolewa kuwa, “Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018, Naibu Waziri wa 
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine 
Ndugulile alikutana na wawakilishi wa vyombo vya habari na kutoa maagizo
 yakuyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taalifa zao kwa 
Mashirika hayo ikiwa ni pamoja na taarifa za miradi na taarifa za fedha 
zilizo kaguliwa kwa mwaka 2017 na 2018”, alibainisha DKT. Jingu.
Dkt
 Jingu amefafanua kuwa, maagizo hayo yalipaswa kutekelezwa ndani ya siku
 thelathini (30) kuanzia tarehe 28.9.2018 ya agizo lilipotolewa na 
Serikali. Hata hivyo imeelezwa kuwa mwitikio wa utekelezaji umekuwa wa 
kuridhisha kutokana na ukweli kuwa Mashirika mengi yamezingatia 
maelekezo ya Serikali.
Aidha,
 Wizara imepokea maombi kutoka Ofisi ya Baraza la Taifa la NGOs na 
baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakiomba kuongezwa muda kidogo 
ili waweze kukamilisha maandalizi ya taarifa zao na kuziwasilisha 
haraka. 
Kutokana na kutambua nafasi ya NGOs katika maendeleo ya Taifa, Serikali imeridhia kuongeza siku kumi na nne (14) kuanzia leo (31/10/2018) ili kuwapa fursa wale ambao walikuwa bado hawajatimiza maelekezo hayo kutokana na sababu mbalimbali kufanya hivyo.
“Nasisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza kwa wale ambao hawatakuwa wamewasilisha taarifa hizo ndani ya muda wa nyongeza. Shirika ambalo litakuwa halijawasilisha taarifa Wizara itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria”. alisisitiza Dkt. Jingu.

Katibu
 Mkuu huyo amerudia kuhakikishia umma kuwa, Serikali inatambua na 
kuthamini mchango wa NGOs kwa maendeleo ya nchi. Msisitizo wa Serikali 
wa uwazi na uwajibikaji unalenga kuwezesha Serikali, wananchi na wadau 
wa maendeleo kutambua vizuri zaidi mchango wa NGOs  katika shughuli za 
maendeleo.
Pia kama ilivyo kwenye sekta nyingine, uwazi na uwajibikaji utasaidia kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali zinazotolewa na wadau wa maendeleo kupitia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuwa kichocheo katika kufikia azma ya maendeleo jumuishi.

Akizungumza
 katika Mkutano huo, katibu Mkuu wa Braza la Mashirika Yasiyo ya 
Kiserikali Bw. Ismail A. Suleiman ameishukuru Serikali kwa kuridhia ombi
 nyenyekevu la kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za fedha na miradi 
ili  kuwezesha NGOs kutimiza takwa la  agizo hio.
Bw.
 Ismail amebainisha kuwa kanuni mpya za NGOs (2018) zilizotangazwa 
tarehe 19/10/2018 kwa kiasi kikubwa zimezingatia utekelezaji wa kanunni 
za maadili; hivyo Braza la NGOs litaunda kikosi kazi kuzipitia na kutoa 
maoni kwa lengo la kuboresha utendaji wa NGOs kwa mujibu wa matakwa ya 
kisheria, kanuni na taratibu.
Baraza
 la NGOs limewataka wanachama wake wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali 
kuhakikisha kuwa wanatekeleza kazi zao kwa mujibu wa katiba za mashirka 
yao ili kushirikiana na Serikali katika kuchochea ustawi na maendeleo ya
 watu hususan kunufaisha makundi yote ya kijamii.
Maagizo
 haya kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanakuja mwezi mmoja baada ya 
AGIZO LA Serikali kutolewa likizitaka NGOs zote nchini pamoja na mambo 
mengine kuwasilisha taarifa zao za kazi na matumizi ya fedha ya miradi 
wanayoitekeleza. 
Imeelezwa kuwa hadi taarifa hii inatolewa zaidi ya Mashirika 2000 yamewasilisha taarifa zao na wengi wanaendelea kuitiki maelekezo hayo.
Imeelezwa kuwa hadi taarifa hii inatolewa zaidi ya Mashirika 2000 yamewasilisha taarifa zao na wengi wanaendelea kuitiki maelekezo hayo.

No comments:
Post a Comment