Mkutano wa 13 wa Bunge unaanza leo, huku miswaada ya sheria mitano ikitarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza ikiwemo wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018.
Spika
wa Bunge, Job Ndugai leo amesema miswada mingine ni wa maji na usafi
wa mazingira, marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2018,
muswada wa mamlaka ya hali ya hewa wa mwaka 2018 na wa mamlaka ya
usimamizi wa usafiri wa nchi kavu.
"Pia
kuna muswada wa sheria za huduma ndogo za fedha wa mwaka 2018 ambao
utasomwa katika hatua zake zote. Hati ya dharura ya mheshimiwa Rais
nimeshaipokea na kamati ya uongozi imeridhia kusomwa katika hatua zake
zote," alisema.
Aidha,
alisema wabunge wanne watakula kiapo kesho ambao wote ni wa CCM,
Thimotheo Mzava (Korogwe Vijijini), Mwita Waitara (Ukonga), Julias
Kalanga (Monduli) na Zuberi Kuchauka (Liwale).
Alisema
pia katika mkutano huo mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa mwaka
2019/20 utajadiliwa na sehemu kubwa mijadala itajikita katika mpango
huo.
Ndugai aliongeza kuwa, maswali 125 yataulizwa na ya papo kwa waziri mkuu yatakuwa 16.
No comments:
Post a Comment