Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kimeondoka alfajiri ya
jana kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya
Lesotho katikati ya mwezi huu kwa ajili ya kufuzu Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, nchini Cameroon.
Kikosi
hicho kimeondoka kikiwa na matumaini makubwa kwamba mazoezi
watakayoyafanya yatawasaidia kuibuka na ushindi mchezo wao ujao dhidi ya
Lesotho ugenini.
Taifa
Stars watakuwa wageni wa Mamba wa Lesotho Novemba 18, mwaka huu, Uwanja
wa Setsoto mjini Maseru, katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ya
mwakani, itakayofanyika Cameroon.
Kikosi
hicho kitaweka kambi ya siku 10 nchini Afrika Kusini kikijifua vikali
chini ya Kocha wake Mkuu, Mnigeria Emmanuel Amunike na msaidizi wake,
Hemed Morocco.
Wachezaji
waliosafiri na Stars ni pamoja na makipa Aishi Manula wa Simba SC,
Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya wa Yanga SC na
Benedictor Tinocco wa Mtibwa Sugar.
Mabeki
ni Shomary Kapombe, Erasto Nyoni wa Simba SC, Ally ëSonsoí Abdulkarim
wa Lipuli FC, Kelvin Yondan, Gardiel Michael wa Yanga SC, Aggrey Morris
na Abdallah Kheri wa Azam FC.
Viungo
ni Salum Abubakar ëSure Boyí, Mudathir Yahya wa Azam FC, Salum Kimenya
wa Tanzania Prisons, Feisal Salum wa Yanga SC, Jonas Mkude na Shiza
Kichuya wa Simba SC.
Washambuliaji
ni Thomas Ulimwengu aliye huru baada ya kuvunja mkataba na Al Hilal ya
Sudan mwishoni mwa wiki, John Bocco wa Simba SC na Yahya Zayed wa Azam
FC.
No comments:
Post a Comment