Sakata la kukamatwa kwa Mbunge wa Kigoma mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe na kushindwa kupatiwa dhamana jana Oktoba 31, kumemuibua kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe na kudai kuwa wabunge waupinzani waachwe wafanye kazi yao.
Mbowe
ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, amefunguka hayo kupitia
ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo ameandika kuwa, "Mhe Zitto
kasema na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimehusishwa. Wanasiasa wa
Upinzani waachwe wafanye kazi yao, mtuhumiwa asiwe Hakimu. Serikali
ijibu hoja kwa vielelezo, ikilazimu iunde tume huru za uchunguzi na
CHADEMA tutasimama na ACT".
Zitto
alikamatwa na polisi jana saa 5 asubuhi na kupelekwa kituo cha polisi
Oysterbay ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu, kisha kuhamishiwa
kituo kikuu cha polisi ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Liberatus Sabas aliwaeleza wanahabari kuwa wanamshikilia
Zitto kutokana na matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kuhusiana na mauaji
ya askari na raia wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Mpaka
jana usiku kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, mwanasiasa huyo
amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ambalo limesema kuwa ataendelea
kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment