Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Maadili limemfungia maisha
kutojihusisha na soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kimaadili.
Mwenyekiti
wa kamati ya maadili ya TFF, Wakili Hamidu Mbwezeleni alisema Kuuli
akitambua nafasi yake ndani ya shirikisho hilo, alifanya makosa hayo
matatu ambayo kimsingi yanastahili adhabu ya kifungo cha maisha
kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu.
Makosa
matatu ambayo yamemtia hatiani Wakili Kuuli ni kusambaza nyaraka za
shirikisho kinyume na kanuni na taratibu, kutoa maelezo yanayoonesha
kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa kuwapa watu wasiohusika na pia kufanya
vitendo vinavyoshusha hadhi ya shirikisho.
"Uamuzi
huu umechukuliwa kwa kufuata kanuni na taratibu. Hakuna aliyemuonea
Kuuli niliweke hilo sawa," alisema Wakili Mbwezeleni.
No comments:
Post a Comment