SERIKALI
imesema kamwe haitokatishwa tamaa na kauli ya baadhi ya Viongozi na
wanasiasa kuhusu dhamira yake ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimamkati
yenye malengo ya kuleta maguezi ya kijamii na kiuchumi kwa Watanzania.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa
ziara ya kutembelea Kituo cha Redio ya TBC Taifa na tathmini ya utendaji
kazi katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Dkt.
Abbasi alisema tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, Serikali ya Awamu imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya
maendeleo ambayo wadau mbalimbali wa maendeleo wameipongeza Serikai yake
kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa lakini wapo baadhi ya baadhi ya
Viongozi na wanasiasa wachache wamekuwa wakipinga mageuzi hayo pasipo na
kutoa hoja za msingi.
“Mageuzi
yanayoendelea kufanywa hayatakuwa na mwisho, Serikali ya Awamu ya Tano
na Watendaji wote tunaomsaidia Rais John Pombe Magufuli tumedhamiria
kuleta mapinduzi ya kweli kwa kuboresha huduma za msingi kwa wananchi na
tutapokea maoni na ushauri lakini kamwe haturudishwi nyuma na Viongozi
na watendaji wanaopinga mageuzi haya” alisema Dkt. Abbasi.
Akitolea
mfano Dkt. Abbasi alisema mara baada ya Serikali kutangaza dhamira ya
kuanzisha mradi wa kihistoria wa kufua umeme wa Stiegler’s Gorge uliopo
Wilayani Rufiji mkoani Pwani wapo baadhi ya wanasiasa na Viongozi
wamekuwa wakipinga mradi huo kwa kigezo cha uharibifu wa mazingira ya
eneo hilo, jambo ambalo lililenga kupeleka taswira hasi kwa wananchi na
wadau mbalimbali wa maendeleo.
Anasema
mageuzi mengine yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na
ujenzi wa ukuta katika machimbo ya madini ya Tanzanite, ambapo kutokana
na hatua hizo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba Serikali
imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha Tsh Milioni 890.
Kwa
mujibu wa Dkt. Abbasi alisema katika kuelekea katika mageuzi ya kijamii
na kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuungwa mkono na
wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na kuweka mfumo imara wa usimamizi
wa fedha za umma ikiwemo makusanyo ya kodi, hatua inayoiwezesha Serikali
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aliongeza
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli itaendelea kutekeleza sera na programu mbalimbali ikiwemo sera
ya elimu bure katika ngazi za elimu ya awali, msingi na sekondari,
ambapo Serikali imekuwa ikitoa Tsh Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya
gharama za uendeshaji wake.
Akifafanua
zaidi alisema kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ukusanyaji wa
kodi, Serikali imeweza kufanya mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali
za kijamii ikihusisha afya, maji, barabara pamoja na ununuzi wa ndege
mpya nne za Serikali na hivyo kufufua upya huduma za Shirika la ndege
Nchini (ATCL) ambazo zilisimama kwa kipindi kirefu.
Akianisha
mafanikio ya ATCL, Dkt. Abbasi anasema moja ya mageuzi makubwa
yaliyofikiwa kwa sasa na shirika hilo ni pamoja na ongezeko la abiria
kutoka abiria 3000-4000 kwa mwezi ambapo kwa sasa wateja wanaotumia
Ndege za Shirika hilo wamefikia 30,000 kwa mwezi.
“Mpaka
sasa tuna ndege nne za Serikali, na mwezi Desemba tutapokea ndege
nyingine 2 aina ya Airbus na mwakani (2019) mwezi Oktoba tutapokea ndege
nyingine 1 na kuzifanya ndege mpya za Serikali kufikia saba, na hivyo
kufanya sekta ya uchukuzi kuwa katika mabadiliko makubwa ya utendaji na
uendeshaji” alisema Dkt. Abbasi.
No comments:
Post a Comment