Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema licha ya ushindi
mkubwa wanaoendelea kuupata kwenye chaguzi mbalimbali, lakini hawatakua
tayari kuwarudisha viongozi mizigo kwa wananchi katika uchaguzi mkuu
mwaka 2020.
Polepole
aliyasema hayo leo Jumanne Novemba 6, 2018 wakati akizungumza na
wajumbe wa kamati za siasa mkoa na wilaya ya Kusini Unguja visiwani
Zanzibar katika ukumbi wa mkutano wa TC Dunga.
Alisema
wabunge na madiwani pamoja na wawakilishi wa CCM wanapaswa kujitathmini
wakifahamu wana jukumu kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi.
"Chama
chetu hakikuwapa nafasi ya uongozo kama zawadi ili mwende mkale bata,
tumewapa nafasi ya kuwatetea wananchi wenu na kutetea ilani ya chama
chetu" alisema.
Pamoja
na hayo, Polepole aliwataka watendaji wa Serikali wakiwamo wakurugenzi
wa manispaa na viongozi wengine wa wilaya na mikoa kuhudhuria vikao
vyote vya chama kueleza utekelezaji wa ilani ya chama katika majukumu
yao.
Alisema haiwezekani kuona wana CCM wanafanya kazi halafu kuna watendaji wanashindwa kuwajibika ipasavyo.
Polepole alisema watendaji hao wanapofanya vibaya lawama kubwa inawenda kwenye chama ambacho ndiyo chenye kutekeleza ilani yake.
Target Alcoholism, Drug abuse, and also Problems. https://imgur.com/a/AOYq1n3 https://imgur.com/a/IUV0LXA https://imgur.com/a/kILoj8I https://imgur.com/a/yNTlEEz https://imgur.com/a/0gmaASn https://imgur.com/a/fQwARmD https://imgur.com/a/Vh4TJHd
ReplyDelete