Wabunge
wasumbufu wanapokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge, wamepatiwa mwarobaini
baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kusema anaweza kuwaona wabunge wote
ukumbinu kupitia kwenye kifaa maalumu kilichofungwa kwenye meza yake.
Ndugai alisema hayo bungeni Dodoma jana alipokuwa akiendesha kikao cha 13 cha Bunge la 11.
Wakati
Waziri Kivuli wa Fedha, Halima Mdee akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi
ya Upinzani bungeni juu ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa
na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20, Ndugai
alionekana kukemea wabunge waliokuwa wakipiga makofi kwa kutumia vitabu.
“Waheshimiwa
wabunge siyo busara kutumia vitabu kupiga makofi, halafu mnatumia
kitabu chenu (cha hotuba ya kambi ya upinzani) hiki.
“Siyo vizuri tumieni mikono, nawaona wote uipitia hiki kifaa hapa,” alisema Ndugai.
Pia katika kikao hicho cha asubuhi, kuna wakati wabunge walikuwa wakipiga kelele huku shughuli zikiendelea.
Spika
Ndugai aliwakemea akitaja upande (wa upinzani au CCM) wenye kelele
zaidi huku akisisitiza kuwa alikuwa anawaona wabunge hao kupitia kifaa
hicho.
Kifaa
hicho kipo kwenye kiti ambacho Spika ama mtu mwingine anayeongoza kikao
cha Bunge huketi wakati Bunge likiendelea na kikao cha kawaida.
Kifaa
hicho pia kipo eneo la makatibu wa Bunge ambako wakati Bunge likiwa
limekaa kama kamati, Mwenyekiti anayeongoza kikao hicho huketi eneo
hilo.
Jana,
Ndugai alitoa kauli hiyo wakati Bunge likiwa limekaa kusikiliza Waziri
wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, akiwasilisha Mpango wa Maendeleo
ya Taifa na lilipokaa kama kamati ya mipango kusikiliza hotua ya Kamati
ya Bajeti ya ile ya Kambi ya Upinzani.
Ndugai
akiwa ameketi kama Spika na hata alipoketi kama mwenyekiti wa kamati ya
mipango, alionekana akiwakemea wabunge kwa nyakati tofauti huku akisema
alikuwa anawaona kupitia teknolojia hiyo.
Teknolojia
hiyo, mbali na kusaidia kuona wabunge wasumbufu pia itasaidia kuona
haraka Mbunge anayetaka kuuliza swali au kutoa hoja yoyote.
No comments:
Post a Comment