WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amenusirika kupata ajali
wilayani Gairo, Mkoani Morogoro baada ya basi la Hekima za Mungu
kuovateki katika kona wakati gari la waziri huyo likiwa eneo sahihi.
Tukio hilo lilitokea jana saa 6:04 mchana wakati Waziri huyo alipokua anatokea Mjini Dodoma kuelekea Jijini Dar es Salaam, katika eneo la nje kidogo ya Mji wa Gairo, basi hilo likiwa mwendokasi likiovateki katika kona, ndipo dereva wa gari la Waziri Lugola alipunguza spidi ili kuiepuka ajali hiyo.
Hata
hivyo Basi hilo lilipopita, Waziri huyo aliekeza gari hilo lifuate kwa
nyuma mpaka walikamate, hata hivyo Basi hilo lilikamatwa na dereva wa
basi hilo kukaguliwa kama alikua na sifa ya kua dereva.
Bara
baada ya kumkagua dereva huyo, Waziri Lugola alizungumza na abiria wa
basi hilo lenye namba za usajili T140 AZZ ambalo lilikua linatoka Dar es
Salaam kuelekea Mjini Kahama mkoani Shinyanga.
“Kwanini
mnashindwa kukemea hii tabia ya huyu dereva, mnataka awaue?, alitaka
kusababisha ajali mbaya sana hapa, nanyi mmekaa kimya, mnafanya makosa
kutokuripoti hii tabia mbaya kabisa,” alisema Lugola.
Aliongeza
kua, yeye ni Waziri ambaye anakemea mwendokasi na kiuwataka madereva
nchini waendeshe kwa umakini, lakini dereva huyo anashindwa kufuata
sheria za usalama barabarani, hivyo anapaswa kuchukuliwa hatua na iwe
fundisho kwa madereva wenye tabia kama hiyo.
Licha
ya Dereva wa Basi hilo, Isaac Vian alikiri kosa hilo na kuomba msamaha
lakini Waziri Lugola aliekeza akamatwe lakini atakapofika mwisho wa
safari.
No comments:
Post a Comment