Serikali
imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu yake kwa
weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa
wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Kampuni
mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini zimeitikia wito wa Serikali
wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa
hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na ziada jambo
litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili
kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo jumatatu tarehe 29 Octoba 2018 na Waziri wa kilimo
Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa
Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.
Waziri
Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini Juma
Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth
Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina
utaratibu huku akiwataka kusimamia kwa weledi ufanisi katika uongezaji
wa uzalishaji wa sukari nchini.
Aidha,
Dkt Tizeba alisema kuwa ufungashaji wa sukari kwenye ujazo wowote ule
kwa kutumia vifungashio vya aina yoyote kama vile mifuko yenye nembo ya
SUPER FINE lazima uzingatie Sheria ya Sukari Namba 26 ya Mwaka 2001
ambayo inazuia ufungashaji wa sukari bila kupata idhini ya Bodi ya
Sukari Tanzania.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa Sheria hiyo ni marufuku kufungasha au kuuza sukari
nyeupe kwa kuwa sukari hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani kama
malighafi na sio kwa ajili ya matumizi ya kawaida majumbani.
Alisisitiza
kuwa Mtu yeyote atakayebainika kuvunja Sheria hiyo ya Sukari,
atawajibika kulipa faini ya kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi
Milioni Kumi (10,000,000) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela au vyote
kwa pamoja.
“Kuna
watu wanaolipa kodi ili wazalishe sukari lakini inapoingia sukari
ambayo imepenya kinyemela hata ulinganifu wa soko madukani unakuwa mdogo
kwa kuwa wanaoingiza bila utaratibu wanauza kwa kiasi cha chini kwa
kuwa hawana uchungu wa kulipa kodi”
“Na
hili sio jambo la hiara Bodi ni lazima isimame kidete kubaini mianya
yote ya wafanyabiashara wanaoingiza sukari bila utaratibu” Alikaririwa
Dkt Tizeba
Kuhusu
sukari ya viwandani (Industial Sugar) Dkt Tizeba alisema kuwa,
wafanyabiashara wamekuwa wakiomba kiwango kikubwa cha kibali cha
uagizaji wa sukari lakini serikali ikihakiki kupitia kodi waliyolipa
inakuwa haifanani na kiasi kilichoagizwa.
No comments:
Post a Comment