Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ametangaza kuwa hatagombea tena uongozi wa chama chake cha Christian Democratic Union -CDU, na kwamba muhula wa sasa wa ukansela ambao ni wa nne madarakani utakuwa wa mwisho.
Ameyasema
 hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama 
chake jijini Berlin, ambapo amesema kuwa muda umewadia wa kufungua 
ukurasa mpya.
Merkel
 mwenye umri wa miaka 64 amekuwa mwenyekiti wa chama cha CDU tangu mwaka
 2000, na Kansela wa Ujerumani tangu mwaka 2005 ambapo katika kipindi 
cha miaka 13 kama Kansela, amekuwa pia mwanasiasa maarufu barani Ulaya.
Aidha,
 Merkel amegusia mivutano ya ndani ya vyama vinavyounda mseto wa 
serikali anayoiongoza, ambayo imesababisha mzozo baada ya mwingine, na 
kuhitimisha kwamba taswira inayotoka katika serikali hiyo haikubaliki.
“Kwa
 uamuzi huu najaribu kuchangia katika kuiwezesha serikali ya Ujerumani 
kujikita katika juhudi za uongozi bora, suala ambalo wananchi wamekuwa 
wakidai, kitu ambacho ni haki yao, hatua hii vile vile inakwenda 
sambamba na azma ya serikali ya Ujerumani kufanya tathmini ya nusu 
muhula, kuhusu ilivyotekeleza majukumu yake, kama ilivyokubaliwa na 
vyama vya CDU, CSU na SPD katika mkataba wa kuunda serikali ya mseto.” 
amesema Merkel
Hata
 hivyo, mwanasiasa huyo wa Ujerumani ambaye alikuwa akichukuliwa kama 
mwanamke mwenye nguvu zaidi duniani, na mwenye kauli ya mwisho katika 
Umoja wa Ulaya, alianza kupoteza ushawishi baada ya uamuzi wake wa 
kuruhusu wakimbizi zaidi ya milioni moja kuingia nchini Ujerumani mwaka 
2015.






No comments:
Post a Comment