WAFUGAJI MJINI KAHAMA KUZINGATIA SHERIA ZA UFUGAJI


Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga imewataka wafugaji wa mifugo katika maeneo ya Mjini kuzingatia sheria ya ufugaji huo ikiwamo kutoathiri jamii inayowazunguka.

Akizungumza na Kahama fm, Afisa mifugo wa halmashauri hiyo, COSTANTINE LUGENDO amesema ufugaji wa mifugo mjini ni lazima uwe wa ndani na kwamba wawe na eneo la kutosha ili mifugo isizurure ovyo.

LUGENDO amesema tayari halmashauri hiyo imeanza kuwachukulia hatua za kisheria wafugaji wanaokiuka ufugaji huo huku ikiwashauri shughuli za ufugaji wa mifugo zifanyike katika maeneo ya vijijini.

Nao baadhi ya wananchi mjini Kahama wamesema wataalam wa mifugo wanapaswa kufanya mikutano ya hadhara na wananachi kwaajili ya kuwaelimisha kabla ya kuchukua hatua za kisheria ili kila mfugaji awe na uelewa wa kutosha juu ya ufugaji wa mjini.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive