Profesa
Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya siasa amesema kuna njama za kukinyima ushindi chama hicho
katika uchaguzi wa ubunge wa Liwale utakaofanyika Jumapili Oktoba 13,
2018.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 9, 2018, Lipumba amesema
Liwale ni ngome ya CUF lakini wameanza kunusa harufu ya kupokwa ushindi.
“Mgombea
wetu Mohamed Rashidi Mtesa anakubalika na tangu achaguliwe kuwa diwani
kata ya Liwale amefanya mengi na hata kushirikiana na watendaji wa
Serikali ila kwa sasa tumeanza kuhisi kufanyiwa rafu, tunaiomba tume
(Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC) itende haki," amesema Lipumba.
Amesema
katika kudhihirisha kuwa Liwale ni ngome ya chama hicho, katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CUF ilishinda kata 17 na CCM kata saba.
Amedai kuwa CCM inataka kulichukua jimbo hilo kwa nguvu kwa kuwatumia baadhi ya watumishi wa umma.
Amesema
si vyema Taifa wakati likiadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha
Mwalimu Julius Nyerere, likaingia kwenye vurugu za uchaguzi Liwale.
“Tufanye
uchaguzi wa haki ili mshindi apatikane kwa haki. Liwale ni ngome yetu
na hiyo inatokana na mizizi iliyowekwa na muasisi wa chama chetu Mzee
Shaban Mloo.
"Mawakala
wetu wamekula viapo lakini mpaka sasa hakuna hata mmoja aliyepewa
nakala za viapo hii ni dhahiri kwamba kuna njama ambazo zinafanyika
kutowapitisha ili wajitangazie ushindi kwa kuiba kura"
"Tunamtaka
Mkuu wa Mkoa wa Lindi aache mara moja tabia ya kufanya mikutano ya
hadhara kwa madai anahamasisha maendeleo na kuwataja wanachama wa CUF
kuwa atawakamata kwa sababu yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama " Amesema Prof Ibrahim Lipumba
Uchaguzi
Liwale unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya
CUF, Zuberi Kuchauka kujiuzulu na kujiunga na CCM. Kuchakua ni mgombea
wa CCM katika uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment