Jeshi
 la Polisi Mkoa wa Mwanza limewaua majambazi wawili katika mapambano ya 
majibizano ya kurushiana risasi na majambazi hao huko katika Lodge ya 
Vatican iliyopo Mtaa wa Calfonia –Nyegezi kata ya Nyagezi Wilaya ya 
Nyamagana Jiji na Mkoa wa Mwanza.
Tukio
 hilo limetokea tarehe 07/10/2018 majira ya saa 23:40hrs, hii ni baada 
ya kupatikana kwa taarifa toka kwa wasiri kwamba hapa Mkoani Mwanza 
wameingia majambazi wawili wakiwa na silaha za moto kwa ajali ya kufanya
 uhalifu na wamefikia Vatcan Lodge iliyopo mtaa Calfonia –Nyegezi. 
Majambazi
 hao baada ya kufika kwenye Lodge hiyo walichukua chumba namba tano na 
kuweka mabegi yao kisha waliondoka kwenda maeneo ya katikati ya Jiji la 
Mwanza kwenye eneo ambalo walipanga kuja kufanya tukio la kiuhalifu. 
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo Polisi tulikwenda mapema katika 
Lodge hiyo kisha tuliweka mtego.
Aidha
 ilipofika majira tajwa hapo juu, Polisi tulikwenda hadi kwenye chumba 
namba tano ambapo walifikia majambazi hao kisha tuligonga mlango mara 
kadhaa tukiwataka majambazi hao wafungue mlango ili tuwakamate wakiwa 
hai lakini waligoma. Ndipo baadae jambazi mmoja alifungua mlango ghafla 
kisha alifyatulia askari risasi, lakini kutokana na umahiri wa askari 
wetu waliweza kumpiga risasi jambazi huyo na kufariki dunia papo hapo.
Wakati
 jambazi huyo amepigwa risasi na askari, jambazi mwingine aliyekuwa 
ndani ya chumba alifunga mlango kisha alivunja dari ya lodge na 
kujificha kwenye dari hiyo. 
Polisi
 tulivunja mlango na kuingia ndani ya chumba hicho kisha alipelekewa 
moto mkali humohumo ndani ya dari ndipo baada ya kuona moto umekua mkali
 jambazi huyo alivunja paa la Lodge hiyo kisha alitoka na kuruka ukuta 
na kuanza kukimbia.
Polisi
 tulifyatua risasi kadhaa hewani na kumuamuru jambazi huyo asimame 
lakini alikaidi amri hiyo, ndipo baadae jambazi huyo alipigwa risasi 
wakati akiendelea kukimbia umbali wa mita mia moja toka ilipo lodge na 
kufariki dunia papo hapo.
Aidha
 katika tukio hilo, Polisi tumefanikiwa kukamata silaha moja 
iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za silaha aina ya short gun 
(Home made gun). Pia upekuzi ulifanyika katika chumba walichofikia 
majambazi hao na kupata risasi tano za silaha aina ya short gun ambazo 
hazijatumika.
Jeshi
 la Polisi Mkoa wa Mwanza, linatoa wito kwa wananchi kuwa waendelee 
kutupatia taarifa, watu wote wanaongia hapa Mkoani kwetu lakini 
haijulikani shughuli wanayoifanya watupatie ili Polisi tuweze 
kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria. Pia tunatoa onyo kwa majambazi 
kwamba Mwanza wataingia lakini hawatatoka, hawa wameingia lakini 
hawajatoka.






No comments:
Post a Comment