Zoezi
la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula
unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa
kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi
ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.
Pamoja
na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana
na hali ya msimu wa mwaka Jana kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo
lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.
Katika
hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi
ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba
2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma
kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.
Katika
ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya
Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa
kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi
kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani
6000.
Ili
kuimarisha dhana ya Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi
kupitia vyama ya Ushirika na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS
ambazo jumla yake zinakuwa 23 ambazo ndizo zilizobainishwa na uongozi
wa Mkoa wa Ruvuma.
Vikundi
hivyo vya wakulima ni kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,
Songea vijijini, Mbinga mji, Mbinga vijijini, Namtumbo na Wilaya ya
Nyasa.
Vumilia
alionyesha kuridhishwa na hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na
kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea kusisitiza na kununua mahindi
yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya
Chakula.
Katika
hatua nyingine Bi Vumilia amewapongeza watumishi wa NFRA kwa kazi nzuri
ya kiuweledi wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao na wakala kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment