Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka
viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kuhakikisha wanafunzi
wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya
kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba.
Ole
Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi
hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa
ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale
wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
“Hakikisheni
watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko
wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa
wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “ alisisitiza Naibu waziri Ole
Nasha.
Kiongozi
huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi
yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna
kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.
“Wazazi
msiwe sehemu ya kuchangia watoto wenu kwenda mjini kwa kuwa tu
wanawatumia fedha kwa ajili ya matumizi bali hakikisheni mnawasimamia
vyema watoto hao katika kipindi chote cha kusubiri matokeo na kuwapeleka
shule pindi matokeo yanapotoka na kuonekana wamefaulu,” alisisitiza
Naibu waziri Ole Nasha.
No comments:
Post a Comment