Marwa Itembe (28), mkazi wa kijiji cha Mbalimbali wilayani Serengeti Mkoa wa Mara amefikishwa mahakamani kwa makosa matatu ya uhujumu uchumi.
Mbele
ya Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile, mwendesha
mashtaka wa Polisi, Paskael Nkenyenge jana Jumanne Oktoba 9, 2918
alisema mshtakiwa alikamatwa na miguu miwili ya nyumbu yenye thamani ya
Sh1.4milioni.
Akisoma
hati ya mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi namba 111/2018 alisema
kosa la kwanza ni kuingia ndani ya hifadhi ya Taifa, la pili ni
kupatikana na silaha za jadi panga na kutega wanyamapori ndani ya
hifadhi kinyume cha sheria.
Alisema
kosa la tatu ni kumiliki nyara za Serikali baada ya kukutwa na miguu
miwili ya mnyamapori huyo ikiwa na thamani ya Sh1.4milioni kinyume cha
sheria.
Ametenda makosa hayo Oktoba 7, 2018 katika eneo la Nyamburi ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote na amerudishwa mahabusu hadi Oktoba 23, 2018 kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment