Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kijiji cha Tabaruka wilayani Sengerema wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye kisima kilichopo kijijini hapo.
Mkuu
 wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amewataja watoto hao kuwa ni 
Given Aloyce (14) na Tekla Aloyce (12) waliokuwa wakisoma shule ya 
Msingi Tabaruka.
Kipole
 amesema tukio hilo limetokea Septemba 29, 2018  saa 11:00 jioni 
kijijini hapo walipokwenda kwenye kisima kufua sare za shule.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema hajapata taarifa hizo lakini anafuatilia.






No comments:
Post a Comment