Mfanyabiashara
 maarufu Tanzania, Dk. Regnald Mengi ametambulisha ujio wa kampuni yake 
mpya ambayo itakuwa ni ya kwanza Tanzania kwa kutengeneza bidhaa 
mbalimbali za Kielektroniki, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi, simu 
janja (Smartphones), computers, Ipads, music bluetooth speakers, 
headphones, earphones .
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dk Mengi amesema simu ambazo zitatengenezwa zitakuwa zinakaa na charge kwa zaidi ya wiki moja zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hasa vijijini pia aina hizo za simu zitatumika kama power Bank kucharge simu zingine.
Aidha
 ameeleza kuwa wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 2000 rasmi na zisizo 
rasmi na kampuni itatoa kipaumbele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye 
sifa stahiki
 






No comments:
Post a Comment