Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wakili Revocatus Kuuli amejiuzulu wadhifa huo.
Kuuli
amefikia hatua hiyo kwa kumuandikia barua Rais wa TFF, Walace Karia
iliyoeleza kujiuzulu nafasi ya Uenyenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa
TFF.
Kuuli
ameeleza sababu ya kufanya maamuzi hayo ni kutokana na kuingiliwa
majukumu yake ya kazi na katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao.
Hivi
karibuni Kuuli alitangaza kuupiga STOP mchakato wa uchaguzi wa klabu ya
Simba baada ya kubainika ulikuwa na mapungufu kadhaa, na baadaye Kaimu
Katibu Mkuu, Wilfred Kidao akamjia juu.
Kidao
alikuja na kumtaka kuandika barua ya maelezo ikimtaka aeleze maamuzi
hayo ameyatoa wapi huku akipewa siku tatu pekee awasilishe majibu.
Baada
ya kupewa amri hiyo Kuuli alimjia juu pia Kidao na kueleza kuwa hawezi
kuingiliwa katika majukumu yake na mpaka imepelekea atangaze maamuzi ya
kuachia ngazi.
No comments:
Post a Comment