Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na kiongozi wa Korea kaskazini
Kim Jong UN wamekubaliana kupanga mkutano wa awamu ya pili kati ya
Marekani na Korea kaskazini haraka iwezekanavyo, ofisi ya Rais wa Korea
kusini ilisema Jumapili.
Tangazo
hilo lilikuja muda mfupi baada ya Pompeo alipowasili Seoul kufuatia
ziara yake ya siku nne kuelekea Korea kaskazini mahala ambapo alikutana
na Kim.
Pompeo
alisema Marekani na Korea kaskazini walikubaliana kuendeleza mazungumzo
na kuchagua tarehe maalumu pamoja na mahala ambako mkutano ujao
utafanyika kulingana na taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Korea kusini,
Moon Jae-In.
Moon
alimshukuru Pompeo kwa ziara yake na aliwatakia mafanikio mema kwenye
mkutano ujao kati ya Kim na Rais Donald Trump wa Marekani.
Viongozi hao wawili walikutana mara ya mwisho mwezi June mwaka 2018 huko Singapore.
No comments:
Post a Comment