Watu
wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Manyara baada ya
kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Mirungi kilo tano sawa na
mabunda 14 yakisafirishwa kutoka mkoani Arusha kwenda Babati.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema watuhumiwa hao
wamekamatwa Oktoba 6-2018 Majira ya saa 12 Jioni katika kituo cha
ukaguzi wa magari eneo la Minjingu kata ya Nkaiti wilaya ya Babati
wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye miili yao maeneo ya
tumboni hadi mgongoni.
Amewataja
waliokamatwa ni Aisha Mohamedi [38] mkazi wa Endasaki, Amani Hassan
[30] mkazi wa Sakina Arusha ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo
hiyo iliyokuwa imefungwa kwenye magazeti na kuwekwa gundi ya karatasi
na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa.
Senga
amesema Watu hao walikamatwa wakiwa katika gari kampuni ya Makara
yenye namba za Usajili T 128 -PDC Fuso wakiwa wamejifunga madawa hayo
kwa mabunda madogo madogo 14 wakiwa wamejizungushia tumboni ili
kuonekane ni mtu mwenye vitambi au mwenye ujauzito na muda wowote
watapandishwa kizimbani.
Ikumbukwe
kwamba Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana wengi kiafya
kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya kazi , hivyo kulazimika
kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kamanda
amewatahadharisha wakazi wa mkoa wa Manyara na wanaoingia katika mkoa
huo kwamba Mkoa wake sio mlango wa kupitisha madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment