MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu amewataka
wananchi wa Kibaha Mjini Mkoani Pwani ,wajipange kuchagua viongozi
wepesi kufuatilia maendeleo na kwenda mbio badala ya kuchagua mazezeta
na mananga ,katika uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa- 2019.
Akihitimisha
ziara yake ya siku sita mkoani hapo katika mkutano wa hadhara ,Mailmoja
Samia aliwasihi wasichague watu wazito,wezi na mafisadi bali waweke
viongozi watakaojenga Kibaha .
“Wanasema
mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe ,mimi nikija ninaona kasoro zilizopo
nitakwambieni kuna kasoro lakini warekebishaji ni nyinyi na viongozi
mtakaowachagua “;:
“Mkichagua
wazuri wataondosha kasoro zilizopo haraka lakini mkichagua wazito na
mananga hapa yatazama tuu chini kunyanyuka hayanyanyuki ,kutembea
hayatembei “alisisitiza Samia .
Akizungumzia
suala la ardhi anasema”:; Wakati napita ,mheshimiwa mkuu wa mkoa
alinionyesha eneo kubwa halina kitu chochote nikamwambia mnataka
manispaa ,lakini mbona eneo hili mwitu mtupu hakuna kuendelezwa
akaniambia linamilikiwa na taasisi fulani “
Aidha
,ameitaka wilaya na halmashauri ya Mji huo kukaa chini na taasisi
ambazo zimehodhi maeneo bila kuyaendeleza katika kipindi kirefu ili
ziweze kuingia ubia .
Awali Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka aliomba mji huo upandishwe hadhi na kuwa manispaa kama vigezo vinaruhusu.
Alitaja
changamoto zinazowakabili kuwa ni ,usambazaji wa maji kwenda kwa
wananchi unasuasua kasi iongezwe kwani mji unakua ila maji hayajawafikia
.
”
Eneo la Tamco-Mapinga zaidi ya miaka mitano wapo wananchi walifanyiwa
tathmini lakini hawajalipwa fidia zao ,tunaomba utusaidie wananchi hawa
waweze kufaidika na fidia hizo”alielezea Koka.
Koka
alitaja tatizo jingine ni ucheleweshaji wa nishati ya umeme , kasi ni
ndogo kufika kwa baadhi ya maeneo na wawekezaji ,ameomba uwafikie maeneo
yaliyo katika miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.
Akijibu
changamoto hiyo, Naibu waziri wa nishati ,Subira Mgalu alisema ,
kupitia serikali ipo sheria iliyoanzisha wakala wa nishati ya umeme
vijijini lakini maeneo ya miji sheria ile ilikuwa huwezi kufanya miradi
ya umeme mijini.
“Serikali
ya awamu ya tano kwa makusudi mazima iliona miji ifaidike na raslimali
zinazopatikana kwenye mfuko wa umeme vijijini na kwa maelekezo yenu
tulibuni mradi wa Peri Urban”;alifafanua Subira.
Subira
alisema ,kiasi cha sh. bilioni 82 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo na
sasa hatua iliyopo ni kumpata mkandarasi ili mradi uanze kazi .
Aliwahakikishia
wananchi ambao hawana umeme katika kata ya Mailmoja
,Viziwaziwa,Pichandege ,Pangani, Misugusugu ,Sofu watanufaika na mradi
huo .
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ramadhani Maneno, alisema Pwani ipo salama
na ushindi ni lazima ,iwe jua iwe mvua uchaguzi ujao wa serikali za
mitaa atahakikisha wanashinda
No comments:
Post a Comment