Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, ameongoza ujumbe wa Tanzania ulioshiriki mkutano wa pamoja wa 16 wa mawaziri wa biashara wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika Brussels. Ubelgiji.
Kwenye mkutano huo Tanzania ilisisitiza azma ya kutosaini mkataba wa EPA.
Mbali na mkutano huo, Profesa Kabudi alishiriki mkutano wa 21 wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara wa ACP.
Taarifa
iliyotolewa jana, ilisema mikutano hiyo miwili ilitanguliwa na mkutano
wa makatibu wakuu wa nchi za ACP wanaosimamia masuala ya biashara.
Ilisema
katika mkutano huo, Tanzania ilisema mkataba wa EPA hauwezi kuwa nguzo
au chachu ya maendeleo kama ilivyo katika malengo yake kwa kuwa hautoi
fursa kwa nchi za ACP kukuza sekta ya viwanda na biashara.
Ilisema badala yake mkataba huo una sura ya misaada kutoka EU kwenda ACP na umelenga nchi za ACP kuwa soko kuu la bidhaa za EU.
Taarifa
hiyo ilisema mkataba huo una vikwazo vingi visivyo vya ushuru ambavyo
husababisha nchi za ACP zishindwe kufanya biashara ya bidhaa na huduma
na nchi mbalimbali za EU.
“Tanzania
ilirejea msimamo wake wa awali wa kutosaini mkataba wa EPA hadi hapo
utakapoboreshwa na kuwa na sura ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi.
“Baada
ya Tanzania kutangaza msimamo wake, baadhi ya nchi nyingine za ACP
ziliunga mkono hoja hii na kuhamasisha nchi nyingine zaidi za ACP
zichukue msimamo wa Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.
Ilisema
katika mikutano hiyo Profesa Kabudi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu,
Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Dk. Edwin Mhede na wataalamu wengine waandamizi kutoka Wizara ya
Viwanda, Viashara na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Brussels.
Tanzania
ni miongoni mwa wanachama wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific
(ACP) tangu mwaka 1975. Nchi hizo za ACP zimekuwa na majadiliano na
Umoja ya Ulaya (European Union – EU) kwa lengo na kukuza ushirikiano
miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment