Lugola Awataka Wakuu Wa Idara Kushirikiana Na Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa idara kushirikiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Katavi.


Amesema hayo leo Oktoba mosi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakuu wa idara wa mkoa wa Katavi, alipowasili mjini Mpanda akitokea Kigoma.

Waziri huyo amefanya ziara ofisi za mkoa huo kwa ajili ya kujua ushirikiano wa watendaji wakuu wa mkoa huo pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo.

Waziri Lugola amepolekewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi, Lilian Matinga na baadhi ya maofisa mbalimbali wa polisi mkoani humo.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive