JESHI
la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato
nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata
kiwanda cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa
hiyo bila ya usajili.
Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara wanatafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.
Hali
hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada
ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha
Pombe kali .
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi
Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine
za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki
ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.
Zoezi
la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo
katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile
vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi vikiwa katika
wilaya ya Rombo.
No comments:
Post a Comment