Kesi
ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake
halali, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai
na wenzake wanne, imeshindwa kuendelea kusikilizwa sababu, Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu haina hela ya kuwaleta mashahidi.
Wakili
wa Serikali, Pius Hila akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Vitalis
Peter ameeleza hayo, leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo,
Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Wakili
Hilla amedai walishaita mashihidi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam
lakini wameshindwa kufika kwa kuwa Mtendaji wa Mahakama hakuwa na fungu
la fedha, kwa ajili ya kuwalipa.Ameendela kueleza kwa sasa wamepata
kibali kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama ambacho kinawaelezea kuwa malipo
yatasubiri fedha zitakapoingia lakini mashahidi wameshindwa kuja kwa
gharama zao wenyewe.
"Mheshimiwa
hakimu kutokana na hali hiyo, tunaomba terehe fupi kwa ajili ya
kuendelea na usikilizwaji wa kesi hii," ameeleza Hilla.Kutokana na
maelezo hayo, Wakili wa Utetezi Alex Mgongolwa aliwasilisha maombi
mawili mahakamani hapo.
,"Mheshimwa,
tunaomba jitihada za kuwapata mashahidi hao waliopo nje ya mkoa wa Dar
rs Salaam ziendelee na pia ni rai yetu kwa mahakama upande wa mashtaka
walete mashahidi ambao hawahitaji kuombewa kibali na hawatoki nje ya
mkoa wa Dar es salaam ili Kesi hii iweze kuendelea," amedai Wakili
Mgongolwa.
Kutokana
na hayo, Hakimu Simba amesema, mahakama itazungumza na Mtendaji wa
Mahakama ili kutafuta fedha sehemu yoyote ili mashahidi hao waweze kuja
mahakamani na kutoa ushahidi kwa sababu kesi hiyo ni ya muda mrefu.Kesi
imeahirishwa hadi Oktoba 15 na 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea
kusikilizwa.
Mpaka
sasa ni shahidi mmoja wa upande wa mashtaka, Ayoub Akida(52) ambaye ni
Ofisa Utumishi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), ameshatoa ushahidi wake dhidi ya Gugai.Mbali na Gugai,
washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.
Katika
kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya
hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki
mali zisizoendana na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika
maeneo mbali mbali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali
zisozoendana na kipato chake, analodaiwa kutenda kati ya January 2005 na
Decemba 2015.
Akiwa
ofisa wa umma ameajiriwa na TAKUKURU alikutwa akimiliki mali za zaidi
ya Sh. bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha
sasa
No comments:
Post a Comment