RADIO ONLINE

Friday, 24 May 2013

Rais dkt Shein amtembelea Sheha Aliyetiwa Tindi kali

000000Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuangalia Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na  Tindikali alilomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa  kushoto Dk.Slim Mohamed Mgeni,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] MG 0000Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyetiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa pili kulia Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  source:fullshangwe

AZAM TV NA SUALA LA KUONYESHA LIGI KUU - SIMBA, YANGA HAZINA NIA NJEMA NA SOKA LA TANZANIA




KAMPUNI ya S. S. Bakhressa ilipoanzisha timu ya soka ya Azam FC, viongozi na mashabiki wa klabu kongwe za Simba na Yanga walidhani ni nguvu ya soka.
S. S. Bakhressa ikapiga hatua ya pili kwa kujenga uwanja wa kisasa, Chamazi, Temeke, Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya dhamira ya kufanya mapinduzi ya soka nchini.
Mbali ya kujenga uwanja wa mazoezi (unatumika hata kwa mashindano) na uwanja mkubwa wa kisasa ambao ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, S.S. Bakhressa imeingia hatua nyingine kubwa kwa kuanzisha kituo cha televisheni cha Azam TV.
Moja ya malengo ya Azam TV inayojenga barabara ya Nyerere ni kutumia kiasi cha Sh. 1.5 bilioni kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ikiwa itapata haki ya kuonyesha ‘live’ mashindano hayo, taarifa zinasema Azam TV imejipanga kutoa Sh. 100 milioni kwa kila timu kati ya 14 zitakazoshiriki msimu ujao wa ligi hiyo. Hii ni neema kubwa kwa klabu zote hasa changa.
Hii ina maana sasa angalau kila timu, itaweza kujikimu kwa kiasi chake na kuweka karibu uwiano sawa wa kuchuana na timu zenye uwezo mkubwa wa kifedha kama Simba, Yanga na Azam FC iliyo chini ya kampuni ya S. S. Bakhressa.
Kwa hiyo, timu zisizo na wadhamini mkubwa na ambazo ndiyo kwanza zimepanda daraja kama Ashanti United ya Ilala, Mbeya City ya Mbeya na Rhino ya Tabora na hata zilizopo kama Coastal Union zitanufaika kwa kiasi kikubwa na ujio wa udhamini wa Azam TV.
Timu zilizoshuka daraja za Toto African, African Lyon na Polisi Morogoro zitakuwa zinasikitika neema kuja kwenye ligi wakati zimetupwa nje.
Msimu uliopita tuliiona Toto ya Mwanza ikishiriki kwa tabu ligi hiyo huku wachezaji wake wakilala katika basi wakati mwingine huku chakula pia kikiwa shida. Hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa timu hizi ambazo hazipo chini ya taasisi kubwa kufanya vibaya hasa katika mechi zake za umbali mrefu na wakati mwingine hata zile za katika kituo chake.
Kwa vyovyote vile Azam TV inakuja kuleta ushindani mkubwa siyo katika udhamini tu, bali hata urushaji wa vipindi vya michezo.
Lakini Simba na Yanga zilizoanzishwa kabla ya uhuru ‘zinapanga’ hujuma. Simba wanadai kiasi cha Sh. 100 milioni ni kidogo na hakilingani na hadhi yao na pia hawawezi kulipwa sawa na timu nyingine za ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage amenukuliwa na gazeti moja la michezo akisema anakubaliana na wazo la Azam TV, lakini kiasi hicho cha fedha ni kidogo kwao na hata siku moja timu haziwezi kulipwa haki sawa ya matangazo huku akitolea mfano katika Ligi Kuu ya England.
Kwa upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto amesema hawezi kuzungumzia vitu vya tetesi kwani Azam TV hadi sasa hawajawapelekea taarifa rasmi kuhusu lengo hilo la kuonyeshwa kwa mechi zao msimu ujao.
“Sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumzia jambo hilo, kwani hatujataarifiwa jambo lolote juu ya mpango huo wa Azam TV, wakituletea maombi yao, sisi kama timu tutakaa na kutoa uamuzi,” anasema Kizuguto.
Hii ina maana kwamba, kama Simba na Yanga zitabaki na mawazo hayo, Azam TV inaweza kukwamishwa katika mpango huu na kubaki na ule wa kuonyesha mechi za timu yao tu, kwani lengo lao ni kutangaza biashara zao.
Utaratibu ni kwamba muda ukifika, uongozi wa Azam TV utaomba kibali cha kudhamini Ligi Kuu kutoka Kamati ya Ligi ambayo itapanga kiwango baada ya kuteta na klabu.
Vituo vya TV vikionyesha ‘live’ mechi yoyote ya ligi hupaswa kulipa gharama kufidia kiasi cha watu ambao hawataingia uwanjani na kutumia fursa hiyo kurusha matangazo ya biashara. Azam TV haitazungumza na klabu binafsi.
Lakini kwa desturi za Simba na Yanga, ambazo miaka nenda rudi ni kupanga mikakati ya kuangushana, hata hili zinaweza kukwamisha. Kwa husuda zitaweka mgomo ili mpango huu ufe ili zenyewe zibaki kutawala soka, timu ndogo zibaki zikinyanyasika kama ilivyokuwa kwa Toto African iliyopigana hadi inashuka daraja.
Rai yangu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati ya Ligi ni kwamba, Simba na Yanga zisiachwe kuharibu mapinduzi ya soka yanayoletwa na Azam TV.
HABARI HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI
 
source:shafiii

Wednesday, 22 May 2013

WAFANYABIASHARA WA NAFAKA KAHAMA WAANDAMANA HADI OFISI ZA WILAYA WAKILALAMIKIA TOZO YA USHURU WA MAZAO INAYOTOZWA NA HALMASHAURI.


  
WAFANYABIASHARA WA NAFAKA WILAYANI KAHAMA WAKIWA MBELE YA OFISI YA WILAYA .
 
KAHAMA
Wafanya biashara wa mazao ya mpunga, mahindi na mtama wanaotoka vijiji mbalimbali wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameandamana leo hadi katika halmashauri ya wilaya ya Kahama wakilalamikia kitendo cha halmashauri hiyo kuwatoza ushuru mara mbili.
Wakiongea na redio kahama katika viwanja vya halmashauri hiyo wafanyabiashara hao wamesema wanashindwa kuelewa bei sahihi ya ushuru kwani hulipa shilingi 500 kwa mzabuni wa gulio la uyogo na shilingi 2000 kwa halmashauri.
Wafanyabiashara hao wamesema halmashauri iliweka mzabuni ambaye anapokea fedha kutoka katika gulio hilo  lakini wanapofika njiani wanalipa sh 2000 kwa kila gunia lenye kilo 100 ambapo wamesema wanaumizwa sana na ushuru huo kwani hawapati faida katika biashara zao.
Akijibu Malalamiko Hayo Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri Hiyo Benjamin Onesmo amesema ,wafanyabiashara wanatakiwa kulipa sh 300 tu kama ushuru wa gulio na sh 2000 kwa kila gunia lenye kilo 100 katika halmashauri.
Onesmo amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kutoa ushuru huo huku akiahidi kupeleka suala hilo katika idara husika kwa ajili ya kuliangalia upya na kulipatia majibu sahihi.
Hata hivyo wafanyabiashara hao wameeleza kutoridhishwa na majibu ya Bw Onesmo, hivyo wamesema wanakwenda mkoani kwa lengo la kuonana na mkuu wa mkoa Ally Rufunga ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA

\BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAKIWA WAMEPUMZIKA CHINI YA MITI BAADA YA KUKAA MUDA MREFU BILA KUSIKILIZWA.


WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI WAKIWA NJE WAKIJADILIANA KUFUATIA HALI HIYO.
 
WAANDISHI WA HABARI NAO HAWAKUWA NYUMA KULIA MWENYE NYWELE NDEFU NI MATRIDA BUHEMBA NA KUSHOTO NI WILLIUM BUNDALA.
HAPA NDIPO NINAPOWAPENDEA POLISI WA KAHAMA HAWAKO NYUMA PINDI MATUKIO YA NAMNA HII YANAPOTOKEA.
VIJANA WA I.G.P MWEMA WAKIHAKIKISHA USALAMA UNAKUWA POUWA

HII NDIYO RISITI ILIYOTOLEWA NA MMOJA WA WAFANYABIASHARA HAO AMBAYO AMELIPIA KATIKA GULIO LA UYOGO.
WAFANYA BIASHARA WAKIWA HAWAJUI WAFANYE NINI
GARI ZILIZOKAMATWA ZIKIWA ZIMEEGESHWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA.
POLISI AKIWATAKA WAFANYABIASHARA HAO WAENDE UKUMBI WA MIKUTANO KUONANA NA MKURUGENZI.
WAFANYABIASHARA WAKISUBIRI MLANGO UFUNGULIWE WAINGIE KUZUNGUMZA NA KAIMU MKURUGENZI.
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA BENJAMIN ONESMO.
WAFANYABIASHARA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MUIKUTANO.
MMOJA WA WAFANYABIASHARA AKITOA MAONI YAKE.
MAONI YAKIENDELEA KUTOLEWA KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA YAO.
TANGAZO LA MKURUGENZI KUHUSU KULIPA TSH 2000/= KWA KILA GUNIA.
WAFANYABIASHARA WAKITOKA UKUMBINI BAADA YA MKUTANO KUTOFIKIWA MUAFAKA.
HAPA WAKIJIPANGA KWENDA KWA MKUU WA MKOA MKOANI SHINYANGA.
MIKAKATI IKIPANGWA.
source:kijukuublog

BREAKING NEWSSSSSSSSS,MAITI YAFUKULIWA NA KUZIKWA UPYA BAADA YA KUZIKWA BILA UTHIBITISHO WA DAKTARI,TUKIO LA KUWEKA MASHADA LAFANYIKA MARA MBILI.


HAPA NI WAKATI AMBAPO DR KUTOKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA AKIWA AMEINGIA NDANI YA KABURI KUANZA KUKAGUA MWILI WA MAREHEMU  LUPIMO LUGENZI (37)

KAHAMA
Ama hakika waswahili hawakukosea waliposema ukistaajabu  ya Musa utayaona ya filauni.
Leo katika kijiji cha Ngongwa kata ya Ngongwa wilayani Kahama Mwili wa marehemu Lupimo Lugenzi(37) umezikwa mara mbili baada ya Jeshi la Polisi Kuamuru kufukuliwa Mwili huo kwa madai kuwa umezikwa bila kukaguliwa na Daktari.
Tukio hilo lililojenga taswira ya Pekee katika kijiji hicho limetokea leo jioni katika kijiji hicho nje kidogo ya mji wa Kahama.
Marehemu Lugenzi alipata ajari  jana majira ya saa mbili usiku maeneo ya Kanegere Magereza alipogonga tera la Ng’ombe wakati akiendesha pikipiki iliyokuwa imepakia watu wawili kutoka Ngongwa kuelekea Mwabomba.
Kwa mujibu wa Kaka wa Marehemu Mabala Lugenzi ameiambia Blog hii kuwa Mara baada ya kupata ajali hiyo walikimbizwa hospitali ya wilaya ya Kahama lakini Marehemu Lugenzi alifariki dunia njiani kabla ya kufika Hospitali.
Akiendelea kufafanua Mabala amesema walipoona mdogo wao ameaga dunia waliamua kumrudisha nyumbani kwa ajili ya Maziko pasipo kufika kituo cha Polisi wala mwili kuchunguzwa na Daktari.
Akiendelea kufafanua Mabala amesema mara baada ya kumaliza kuzika na kuweka mashada ya maua walishangaa kuona Polisi wakiwasili na Daktari na kuwaamuru wafukuwe mwili huo ili ufanyiwe uchunguzi kwa mujibu wa sheria.
Mara baada ya kukaguliwa Mwili huo na kujiridhisha kuwa kilichomuua ni ajali waliruhusiwa  kumzika upya na hatimaye ndugu na jamaa kuanza kuweka mashada kwa mara ya Pili.
MATUKIO KATIKA PICHA

  
PICHA YA AWALI KABLA YA KUFUKUA MARA YA PILI KABURI HILO NDUGU WAKIWEKA MASHADA YA MAUA.

NDUGU WA MAREHEMU WAKIWEKA MASHADA YA MAUA BAADA YA MAZIKO YA AWALI.
  
KABURI LIKIFUKULIWA MARA YA PILI ILI KUKAGULIWA MWILI WA MAREHEMU
  
WANANZENGO WAKIWA WAMEISHIWA POZI BAADA YA KUKUTANA NA TUKIO KAMA HILO KATIKA MAISHA YAO YOTE.
WATU WAKISHUHUDIA TUKIO HILO.
  
UCHIMBAJI WA KUFUKUA KABURI UKIENDELEA HUKU DR ALIYECHUCHUMAA KAVAA SHATI LA BLUE AKIJIWEKA SAFI KUINGIA KUKAGUA MWILI HUO.
 
UCHIMBAJI UKIENDELEA ILI KULIFIKIA JENEZA

HAPA WAKIFUKIA BAADA YA DR KUTHIBITISHA KUWA KIFO KIMESABABISHWA NA AJALI

  
HAPA WAKIENDELEA KUFUKIA.
ZOEZI LA KUUFUKIA MWILI WA MAREHEMU LIKIENDELEA CHINI YA ULINZI WA MKALI WA POLISI.

  
NDUGU NA JAMAA WAKIWEKA MASHADA YA MAUA KWA MARA NYINGINE.

BAADA YA UWEKAJI WA MAUA KUKAMILIKA MISHUMAA IKAWASHWA TENA.

HALI YA SINTOFAHAMU ILIVYOKUWA KATIKA KAYA HIYO.
 
source:kijukuublog

Monday, 20 May 2013

Rais Obama kutua Tanzania


Rais wa Marekani Barack Obama ambaye anatarajiwa kudhuru Tanzania siku za hivi karibuni  

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa ujio wa Rais Barack Obama wa Marekani nchini, ni fursa nyingine kwa Tanzania kukuza uchumi na kuimarisha uwekezaji.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio wa Rais Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na wataalamu wa masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Ziara yake ya kwanza aliifanya wakati wa awamu yake ya kwanza madarakani, wakati ziara ya safari hii ni kipindi chake cha lala salama.
Rais Obama alianza rasmi awamu yake ya kwanza kama Rais wa Taifa kubwa, Januari 20, 2009, wakati ng’we yake ya mwisho ilianza Januari 21, 2013.
Rais Obama anatarajiwa kufanya ziara hiyo mwishoni mwa Juni mwaka huu, ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za Afrika Mashariki kutembelewa na kiongozi huyo.
Ziara ya Rais Obama inafanyika baada ya ziara ya Rais Xi Jiping wa China aliyeitembelea Tanzania Machi 28, mwaka huu, ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya kwanza kuitembelea kwa Afrika tangu achaguliwe kuwa rais, Machi 14, 2013.
Akizungumzia ziara hiyo tarajiwa, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi, alisema amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa kulinganisha na nchi nyingine za jirani, vimechangia kuwapo kwa ziara hiyo.
Profesa Lipumba alisema pia ugunduzi wa rasilimali za asili kama vile gesi, mafuta na madini ya urani ni sababu nyingine iliyomfanya Rais huyo kuja nchini.
Hivyo aliwashauri viongozi wa Serikali kujipanga kwa ajili ya kufungua mlango huo mwingine wa uchumi na uwekezaji.
Alisema pamoja na hali hiyo pia kuna mambo ambayo yanaweza kuchafua taswira ya nchi kama vile ubovu wa miundombinu ya barabara, msongamano wa magari barabarani na msongamano wa meli bandarini wakati zikisubiri kushusha mizigo.
Jumatano ya wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alitangaza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushirikiano kati ya Marekani na Afrika, kwamba Rais Obama hivi karibuni atafanya ziara Afrika.
Ingawa Kerry hakutoa maelezo zaidi ya nchi gani za Afrika ambazo Rais Obama atazitembelea, lakini baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria vilieleza kiongozi huyo atafanya ziara Tanzania, Rwanda na Nigeria.

source:mwananchi

Vurugu kubwa Iringa, Mchungaji Msigwa mbaroni

Share bookmark Print Email Rating

Polisi wakimwaga maji ya kuwasha katika eneo la Mashine Tatu, Mjini Iringa  kuwatawanya wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo hilo jana. Picha na  Said Ng’amilo.  

Iringa. Mji wa Iringa uligeuka kuwa uwanja wa vita kati ya polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wafanyabiashara jana asubuhi. Watu 50 walikamatwa kutokana na tukio hilo akiwamo Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Katika vurugu hizo, gari la zimamoto lilivunjwa kioo na gari lingine dogo liliharibiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema Mchungaji Msigwa alikamatwa saa saba mchana kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo na kwamba watu wapatao 50 walikuwa wamekamatwa katika fujo hizo zilizochukua karibu saa tatu.
“Mchungaji Msigwa amekamatwa kwa makosa ya uchochezi, kufanya maandamano bila kibali na kuhamasisha watu kufanya biashara kwenye eneo ambalo limekatazwa kisheria.
Tumemkamata na hatutamwachia hadi uchunguzi wa suala hili utakapokamilika. Pia na hao watu wengine,” alisema Kamanda Kamhanda.
Alisema waliamua kufanya doria katika eneo hilo baada ya kupata taarifa za kiitelijensia kuwa wafanyabiashara walikuwa na mpango wa kuwashambulia mgambo wa Iringa kama wangekwenda kuwazuia.
Vurugu hizo zilichangiwa na mvutano uliokuwa unafukuta kwa muda mrefu kati ya Uongozi wa Manispaa na Mbunge huyo kuhusu amri ya kuzuia watu kufanya biashara kwenye Barabara ya Mashine Tatu, Iringa.
Uongozi wa Manispaa ya Iringa ulitoa tangazo Aprili 28, mwaka huu ukipiga marufuku kufanya biashara katika eneo hilo jambo ambalo lilipingwa na Mchungaji Msigwa na wafanyabiashara hao.
Alfajiri
FFU walianza kuimarisha ulinzi katika Barabara ya Mashine Tatu tangu alfajiri jana na wafanyabiashara hao walipofika kwenye eneo hilo walikuta limezingirwa na polisi.
Kusambaa kwa taarifa hizo kulimfikia Mchungaji Msigwa ambaye alifika hapo saa mbili asubuhi na kuanza kuzungumza na wafanyabiashara hao.
Watu walipomwona ndipo wakamzunguka na kuanza kuimba nyimbo za kumsifu na kumshangilia: “Rais wetu... Rais wetu... Rais wetu.”

source:mwananchi

CCM KAHAMA YAPOTEZA MPIGANAJI,NI KUFUATIA KIFO CHA DIWANI WA KATA UBAGWE MH.ROBERT MDULA.


 
ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA UBANGWE KWA TIKETI YA CCM MH.ROBERT MDULA ENZI ZA UHAI WAKE.
KAHAMA
Wananchi wa Kata ya Ubagwe wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wametakiwa kuyaenzi mazuri aliyoyafanya aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Robert Mudula aliyefariki dunia jana mjini Kahama.
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika maziko ya mwili wa marehemu Mudula yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia yaliyoko kijiji cha Ulowa namba tano, wilayani humo.
Akitoa salam za serikali  kwenye mazishi hayo Mpesya amesema Marehemu Mudula alikuwa dira ya maendeleo ya kata ya Ubagwe, hivyo ametaka mazuri aliyoyaacha yawe dira kwa wote waliobaki.
Kufuatia kifo cha Mudula, Chama Cha Mapinduzi wilayani humo kupitia mwenyekiti wake  wa wilaya Mabala Mlolwa, kimemtaja diwani wake wa viti maalumu kutoka kata ya Bulungwa Ester Matone kuwa mwakilishi mlezi wa kata ya Ubagwe.
Mziko ya Marehemu Madula yamefanyika jioni hii huku yakihudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata za Ulowa na Ubagwe, kata ambazo zimegawanywa kwenye uchaguzi wa 2010 kuwa kata mbili.
Wakati huoi huo Mbunge wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga James Lembeli, ametoa salamu za rambirambi kwa wananchi wa Kata ya Ubagwe kufuatia kifo hicho cha Mh.Robert Peter Mudula.

MATUKIO KATIKA PICHA
  
MWILI WA MAREHEMU R.MDULA UKIWA UMEWASILI NYUMBANI KWAKE UBAGWE KWA AJILI YA KUAGWA.


MAANDALIZI YA KUUGWA MWILI WA MAREHEMU YAKIWEKWA SAWA
VIONGOZI WA CCM NGAZI YA MKOA NA WILAYA WAKIPANGA JAMBO KATIKA MSIBA HUO.

DIWANI WA VITI MAALUM KATA JIRANI YA BULUNGWA MH ESTER MATONE ALIYETEULIWA NA CHAMA CHA CCM KUWA MWAKILISHI WA KAYA YA UBAGWE MPAKA PALE UCHAGUZI UTAKAPOKAMILIKA.

MAMA WA MAREHEMU MDULA AKIWA AMESHIKILIWA NA MAJIRANI ZAKE WAKATI WA KUAGA MWILI WA MWANAWE.

KATIBU WA CCM MKOA WA SHINYANGA AKIAGA MWILI WA MAREHEMU.

MWENYEKI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA KAHAMA IBRAHIMU KHAN AKIAGA MWILI WA MAREHEMU.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAHAMA AKIPITA MBELE YA JENEZA BAADA YA KUAGA.

DIWANI WA VITI MAALUMU KATA YA KAHAMA MJINI MH AOKO NYANGUSU AKIAGA MWILI WA MAREHEMU

DIWANI WA WENDELE AKIAGA MWILI WA MAREHEMU.

DIWANI WA KATA YA IGOMANONI AKIAGA MWILI WA MAREHEMU.

AFISA ELIMU NAYE ALIKUWEPO KUMWAKILISHA MKURUGENZI WA WILAYA YA KAHAMA.

MARAFIKI WA MAREHEMU NAO WALIKUWEPO KUMUAGA MWENZAO.

MWL STEVE WA SHULE YA MSINGI IHATA AKIAGA MWILI WA MAREHEMU

MMILIKI NA MWANDISHI WA BLOG HII NAYE ALIKUWEPO KUAGA MWILI WA MAREHEMU

MWANACHAMA WA CCM AKIFUNIKA MWILI WA MAREHEMU MARA BAADA YA ZOEZI LA KUAGA KUKAMILIKA

UMATI WA WATU ULIOFULIKA KUMUAGA MH.MDULA NYUMBANI KWAKE IHATA-UBAGWE

DIWANI WA KATA YA ULOWA MH.PASKALI MAYENGO AKIWA KATIKA MAZISHI HAYO NA PICHA YA MAREHEMU.

KINA MAMA WAKIWA KATIKA MSIBA HUO WA MH.MDULA

MWILI WA MAREHEMU UKIBEBWA KWENDA KWENYE MAZIKO ULOWA NO 5

MWILI WA MAREHEMU UKIPAKIWA KWENYE GARI KUTOKA UBAGWE KWENDA ULOWA KWA MAZIKO

MWILI WA MAREHEMU UKIWASILI NYUMBANI KWAO ULOWA NO 5

KATIBU WA CCM WILAYA YA KAHAM MR.BUNDALA AKIWA KATIKA MSIBA  HUO.

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KAHAMA KULIA MABALA MLOLWA AKITETA JAMBO NA KATIBU WA CCM MKOA WA SHINYANGA.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MH MPESYA KUSHOTO AKITETA JAMBO NA WANAZENGO.

NDUGU WAKIWA WANAWASILI KATKA MSIBA KWA MAJONZI

UMATI WA WATU WAKIWA KATIKA MAZISHI HAYO.

HII NDIYO NYUMBA AMBAYO MAREHEMU MDULA AMEPUMZISHWA.

UKAFUTA MUDA WA KUWEKA MCHANGA  WA KWAHERI.
 
MH BENSON MPESYA AKIWEKA MCHANGA WA KWAHERI

MWENYEKITI WA HALMASHAURI AKIWEKA MCHANGA WA KWAHERI

ZOEZI LA KUWEKA MCHANGA LIKIENDELEA.

DIWANI WA KATA YA ULOWA AKIWEKA MCHANGA

BURIANI MH MDULA



































0 comments:

Post a Comment

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!