DIWANI KAHAMA AANGUA KILIO KWENYE BARAZA LA MADIWANI,AKILALAMIKIA HOJA YAKE KUTOPEWA NAFASI


DIWANI WA KATA YA SABASABINI HALMASHAURI YA USHETU EMMANUEL MAKASHI ALIYEANGUA KILIO KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

Na Salvatory Ntandu
KAHAMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Diwani wa Kata ya Sabasabini EMANUEL MAKASHI amengua kilio  kwenye kikao cha Baraza la Madiwani alilalamikia hoja yake kutopewa nafasi ya kusikilizwa katika kikao hicho  aliyoiwasilisha juu ya kutoridhishwa na utendaji kazi  wa afisa Mtendaji wa Kata hiyo CHRISTOPER LYOGELO.
Katika Madai aliyoyawasilisha MAKASHI amesema tangu afisa huyo apangiwe katika kituo hicho cha kazi mwaka 2005 ,amekuwa hasomi mapatao na matumizi, hali ambayo imesababisha wananchi kugoma kuchangia shughuli za maendeleo.
Baada ya kumsikiliza MAKASHI hatimaye hoja hiyo imejibiwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu ONESMO BENJAMIN  na haya hapa majibu yake aliyoyatoa kwenye kikao.
Amesema watahakikisha suala hilo linafanyiwa kazi kwa haraka ili muafaka upatikane.
Lakini baaada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Baraza la Madiwani Raha ya leo ilimtafuta MH.MAKASHI kuzungumzia hoja aliyoiwasilisha katika Baraza hilo.
Baraza la Ushetu limeketi kwa siku mbili kwa wakilishi wananchi(madiwani) kujadili taarifa mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya wananchi.
Share:

WAZEE KAHAMA WATAJWA KUWA NA NAFASI YA KUIMARISHA MILA NA DESTURI

Wazee  wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wametajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuimarisha mila na desturi katika jamii endapo waataendelea kusimamia  na kuelekeza maadili mema kwa jamii.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na  Katibu wa Umoja wa  wazee wilaya ya Kahama (UWAKA) PAUL NTELYA wakati akizungumza kwenye  Uzinduzi wa tawi la umoja huo kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu.
NTELYA amesema ili kuwa na taifa lenye watu waadilifu ni lazima wazee wachukue nafasi ya kukemea maovu yote yanayoharibu maadili mema katika jamii na kwamba jamii izidi kudumisha mila na desturi zao.
 
Katika huzinduzi huo wa tawi  la UWAKA kata ya Bulungwa, umeundwa uongozi wa  Kata hiyo ambao utaratibu shughuli zote zinazuhusu umoja huo ikiwamo kutetea haki za  wazee hasa katika upande wa matibabu na migogoro ya ardhi.
Mwneyekiti wa UWAKA , Kata ya Bulungwa,  KAGEMO KAYANDA, amewaomba  wazee katika kata hiyo kuwa na umoja ili kuisdaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwamo suala la Migogoro ya Ardhi ambalo limekuwa ni tatizo kubwa katika maeneo mengi nchini.
Share:

BODI YA ELIMU MSALALA KAHAMA YAKABIDHI MADAWATI 160 KATIKA SHULE TATU ZA SEKONDARI

Zaidi ya madawati 160 yamekabidhiwa na bodi ya elimu-Msalala, katika shule tatu za Secondari za halmashauri ya hiyo ili kupunguza tatizo uhaba wa madawati kwa shule za sekondari.
Akizungumza leo katika makabidhiano ya madawati hayo kaimu katibu wa bodi ya elimu Msalala MASATU MNYORO  amezitaja shule zilizokabidhiwa madawati hayo  kuwa ni  shule ya sekondari Segese, Isaka na   Mwalimu nyerere.  
MNYORO amesema  halmashauri hiyo, imekusudia kuboresha sheria  ya  mfuko wa elimu ili iwe na vyanzo vingi vya mapato na kwamba amewataka walimu wakuu  kusimamia utunzaji wa madawati hayo.
Kwa upande wao walimu wakuu wa shule hizo wameishukuru Halmashuri hiyo na kwamba madawati hayo yatasaidia kupunguza changamato ya madawati.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya msalala SIMON BEREGE amewataka wadau mbali mbali kushirikiana kwa pamoja ili kujenga vyumba vya madarasa na madawati ili kuondokana na tatizo hilo.
Bodi ya mfuko wa elimu kwa Halmshauri ya msalala ilianza kufanya kazi mwaka 2016 kwa kuhakikisha inaboresha miundombinu ya elimu na kutafuta fedha kwa ajili ya kutengeneza madawati, kujenga maabara na vyumba vya madarasa.
Share:

SERIKALI: WAANDISHI WA HABARI ACHENI KUCHANGANYA TAALUMA NA SIASA

SERIKALI imewataka waandishi wa habari nchini kutochanganya taaluma zao na ushabiki wa siasa ili kuandika habari zenye tija katika jamii zenye kuleta maendeleo .
Wito huo umetolewa February 13 mjini Dodoma na naibu waziri wa Habari michezo na utamaduni Bi Juliana Shonza katika maadhimisho ya siku ya Redio duniani iliyofanyika kitaifa mjini Dodoma katika ukumbi wa Hotel ya Nasheera.
Akiongea kwa niaba ya waziri wa habari Dr Harrison Mwakyembe,Bi Shonza amesema waandishi wa habari wanapoingia kwenye siasa,hawatoandika habari za mizania hali itakayoleta migogoro katika jamii.
Katika hatua nyingine Bi shosa ametoa wito kwa waandishi wa habari kudumisha mila na desturi hasa katika matumizi ya fasaha ya Lugha ya Kiswahili na kusema kuwa kwa sasa waandishi na watangazaji wengi wanatumia lugha ya Kiswahili na kuchanganya na lugha ya kingereza kwa wakati mmoja.
Naye Katibu wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka serikali kuhakikisha kwamba urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa umma ili kuwezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali vya habari. 
Alitaka Tamisemi kuweka utaratibu wa utoaji habari katika mfumo rahisi ili wananchi wafahamu kinachotekelezwa na serikali yao. Aidha maafisa habari walioajiriwa wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na serikali na wawe na ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika maeneo yao.
Aidha alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali ingeangalia suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za Jamii kutolipia huduma za Radio.
Pia amesema sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya mwanahabari, mfano sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria ya makosa ya mtandao kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa katika mashaka zaidi kuliko kipindi kilichopita. 
Ameongeza kwa kuiomba  Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa wanahabari ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021.
Awali akitoa salamu za Shirika la umoja wa mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni-UNESCO- Kiongozi mkuu wa ofisi ya Shirika hilo Dar es salaam Bi Faith Shayo ametoa wito kwa waandishi wa habari kuandika habari za Usawa wa kijinsia,Maendeleo na zenye kudumisha amani.
Siku ya redio duniani huazimishwa kila mwaka tarehe 13 mwezi wa 2 duniani Pote na kauli mbiu ya mwaka huu ni Redio na michezo.
MATUKIO KATIKA PICHA:  

 
Katibu wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mtandao huo, Prosper Kwigize wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma kwa ufadhili wa UNESCO.
 

 
 
 
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili kushoto) akitoa salamu za UNESCO wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari yaliyofanyika mjini Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche (wa kwanza kushoto).
 
 
Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dk. Moshi Kimizi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Mjini Dodoma.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
 
 
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza akiwasili katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma kushiriki sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa (kushoto).
 
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche wakiwa meza kuu wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani mjini Dodoma.
 
Mratibu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari na Jinsia Kusini mwa Afrika (GEMSAT) , Gladness Munuo akitoa mada kuhusu usawa wa jinsia katika kuripoti michezo, changamoto na taratibu zake wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.  
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akisisitiza umuhimu wa maudhui katika vipindi vya redio ambapo aliwaasa kutangaza masuala yanayowahusu wanajamii katika maeneo yanayohusika badala ya kuwalisha wasikilizaji taarifa ambazo ziko nje na mipaka wanayoishi.
 
Mtaalamu wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano, Mariagoreth Charles akiwasilisha kanuni za uandishi wa habari za mtandaoni na mitandao ya kijamii kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
 
Mtangazaji Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema pamoja na kwamba waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini maudhui hayakidhi na kuvutia vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati akichangia kwa nini waandishi wengi hawaandiki habari za michezo. Majura amesema yeye mwenyewe amewahi kupata tuzo mbili kwa ajili ya vipindi vya michezo.
 
Pichani juu na chini ni sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
 
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa tano kulia) wakicheza wimbo maalum wa ngoma za asili wa Kikundi cha Kaza Roho cha mjini Dodoma ulioongozwa na Msanii Mwinamila wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
 
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Share:

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO KUPATA VYEO NA SIYO KUFANYA MAPENZI NA WAAJIRI

BI ROSE HAJI MWALIMU  AKIWASILISHA MADA KWENYE MAFUNZO YA TATHIMINI NA UFUATILIAJI KWA WANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA 



Wandishi wa habari wanawake nchini  wametakiwa kutumia uwezo wao kitaaluma wanapotekeleza majukumu yao wawapo kazini na si kujiingiza katika masuala ya mapenzi na waajiri wao ili wapandishwe vyeo.

Share:

KUWASA YAPATA HASARA YA SHILINGI MILIONI 106 BAADA YA KUKOSEKANA KWA MAJI MJINI KAHAMA KWA SIKU 12

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama, (KUWASA) imepata hasara ya  takriban shilingi milioni 106 kutokana na ukosefu wa maji ulioukumba mji wa Kahama kwa takriban siku 12.

Hayo yamebainishwa na  Kaimu Mkurugenzi wa KUWASA, Mhandisi  CHANGANYA PAUL katika mkutano wake na Wandishi wa Habari kuzungumzia athari zilizotokana na kusitishwa kwa huduma hiyo na jinsi Mamlaka ilivyojipanga kukabiliana na hali hiyo siku za usoni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa  Bodi ya Wakurugenzi ya KUWASA, Meja Mtaafu BAHATI MATALA amesema wanafanya mazungumzo na KASHWASA ili  kutafuta nishati  mbadala ya umeme kwenye chanzo kikuu cha maji ya ziwa Viktoria kilichopo Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza.


Januari 17 mwaka huu, Shirika la Umeme TANESCO lilisitisha huduma ya umeme kwenye chanzo hicho cha Ihele,  kutokana na  deni la zaidi ya shilingi bilioni mbili wanaloidai KASHWASA  hatua iliyosababisha mji wa Kahama kukosa maji kwa takriban siku kumi na mbili na hivyo uzalishaji wa maji kusimama kabisa.
Share:

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels