WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara ya kushtukiza
katika Kituo cha Polisi Katoro mkoani Geita na kuwahoji watuhumiwa wa
makosa mbalimbali waliokuwepo katika mahabusu kituoni hapo.
Lugola
ambaye alikua safarini kuelekea Mkoani Kigoma kwa ziara yake ya kikazi,
ghafla aliibukia katika kituo hicho akitaka kujua utendaji kazi wa
polisi pamoja na makosa mbalimbali wanayowakabili watuhumiwa waliopo
katika mahabusu hiyo na pia kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili
askari wa kituo hicho.
Lugola
aliowasili kituoni hapo jana mchana na akaelekea moja kwa moja mahabusu
na akaomba kitabu cha taarifa ya makosa mbalimbali yaliyoripotiwa
kituoni hapo, na akamuelekeza askari wa zamu awapange foleni watuhumiwa
hao ili aweze kuwahoji makosa yao na pia Mkuu wa Kituo cha polisi hicho,
aweze kufafanua makosa yao.
Baada
ya watuhumiwa hao, Lugola licha ya kuwapongeza polisi wa kituo hicho
kwa kufanya kazi vizuri, pia alimtaka Mkuu wa Kituo hicho, Steven Kimaro
kua makini na utendaji wake na kuwafuatilia kwa umakini utendaji kazi
wa askari wake kwasababu yeye ndio kiongozi wa kituo hicho.
“Sipendi
wananchi waonewe, haki itendeke na si kila kosa lazima mtuhumiwa awekwe
mahabusu, tumieni busara umakini ili tuweze kutenda haki na pia nataka
jeshi hili liwe na picha nzuri zaidi kwa jamii,” alisema Lugola.
Pia
alifafanua kua, hataki kusikia askari polisi anatuhumiwa kwa rushwa au
kunyanyasa wananchi, na endapo taarifa hizo zitamfikia basi atahakikisha
askari huyo anachukulia hatua za kisheria.
Aidha,
Waziri Lugola alitaka polisi wa usalama barabarani kufuata sheria na
pia si kila kosa lazima mwenye gari kuandikiwa risiti ya malipo, makosa
mengine watoe elimu zaidi kwa madereva hao ili taifa liweze kusonga
mbele.
Lugola
Septemba 25 anatarajia kuanza ziara yake ya kutembelea mikoa yote
nchini, ambapo ataanza ziara katika Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma
ambapo atazungumza na askari na maafisa polisi, watumishi wa taasisi
zilizopo katika wizara yake na baadaye atafanya mkutano wa hadhara kwa
kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao mjini humo.
No comments:
Post a Comment