Mahakama
ya Hakimu Mfawidhi mkoa wa Iringa imefunga kusikiliza ushahidi wa
shauri linalomkabili mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo
baada ya kusikiliza mashahidi wawili wa upande wa utetezi, ambapo
imepanga Oktoba 2 kutaja siku ya kutoa hukumu ya kesi hiyo.
Kabla
ya kufunga ushahidi huo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa Iringa Liad
Chamshama amesikiliza mashahidi wawili wa upande wa utetezi ambapo
shahidi wa kwanza ni Abdul Nondo na shahidi wa pili ni Alphonce
Lusako.
Akitoa
ushahidi mbele ya Hakimu jana Abdul Nondo akiongozwa na wakili wake
Jebra Kambole, Nondo amedai kuwa alitekwa na watu wasiojulikana karibu
na geti la chuo cha maji ubungo majira ya saa tano Usiku, siku ya
tarehe 6 Machi 2018, kwa kuvamiwa na kutupwa siti ya nyuma ndani ya
gari.
Nondo
amesema watu hao walikuwa wakimhoji kwanini anatumiwa na wanasiasa
kiasi cha kuvuruga amani na walimtuhumu kuwa anatumiwa na Mwenyekiti wa
Chadema Freeman Mbowe, Zitto Kabwe na Hellen Kijo Bisimba (aliyekuwa
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu-LHRC) pamoja na
kumshutumu kuwa yeye ni wakala wa Mange Kimambi katika kuandaa
maandamano ya wanafunzi lakini amekana tuhuma hizo.
Kwa
upande wake shahidi wa pili Alphoce Lusako ambaye ni kiongozi mwezake
katika shirika la TSNP ameiambia mahakama kuwa baada ya kupata taarifa
kutoka kwa Paul Kinabo kuwa amepokea ujumbe kwa njia ya simu kutoka
kwa Nondo kuwa yupo hatarini na ndipo wakatoa taarifa kwa uongozi wa
chuo na askari wasaidizi wa chuo na kupewa RB.
Mtuhumiwa
Abdul Nondo alifikishwa Mahakamani Machi 21, 2018 na kusomewa
mashitaka yake ambayo yote aliyakana kuhusika nayo hivyo Oktoba 2 mwaka
huu Mahakama itarejea tena kwa ajili ya kutaja siku ya hukumu.
No comments:
Post a Comment