WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 baada ya Serikali kufanikiwa kudhibiti biashara hiyo.
Ameyasema
hayo leo (Jumatatu, Septemba 17, 2018) baada ya kufungua mkutano wa 28
wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za
Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere(JNICC), unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za
Afrika unatarajiwa kutoka na maazimio ya namna ya kutokomeza biashara ya
dawa za kulevya katika mataifa hizo.
Waziri
Mkuu amesema lengo la mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga
mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya
dawa za kulevya katika nchi hizo.
“Ni
lazima tuwe na mikakati ya pamoja ya kudhibiti uzalishaji, usambazaji
na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika. Hata hivyo ni muhimu
kudhibiti njia zote zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inaendelea na mikakati ya kupambana
na uzalishaji wa dawa hizo ikiwemo mirungi na bangi, ambayo inapandwa
kwa kuchanganywa na mazao ya chakula.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi ya kwanza katika bara la
Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha vituo vya utoaji wa
matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya mwaka 2011.
Amesema
hadi kufikia mwishoni mwa 2017, jumla vituo sita vya kutolea matibabu
vilianzishwa, ambapo zaidi ya waathirika 6,500 wa dawa za kulevya aina
ya heroin walijiandikisha na kupatiwa matibabu.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini
yameathiri sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, uchumi na jamii, uchunguzi
umebainisha kuwa kati ya asimilia 20 hadi 50 ya watumiaji wanamaambuzi
ya ugonjwa wa ukimwi.
Amesema
ni muhimu kwa nchi zote kuunga mkono na kuimarisha mifumo ya kisheria
ya kimataifa katika udhibiti wa biashara za dawa za kulevya, ambao
hutegemea mikataba yote ya msingi ya Umoja wa Mataifa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
No comments:
Post a Comment