Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza tume ya kuchunguza ajali ya Kivuko cha
Mv Nyerere, kilichozama Septemba 20 mwaka huu, Ukerewe jijini Mwanza na
kusababisha vifo vya watu 224.
Majaliwa ameitangaza tume hiyo ya wajumbe saba itakayoongozwa na Jenerali mstaafu, George Waitara leo
Jumatatu Septemba 24, katika Kijiji cha Bwisya, wilayani Ukerewe
alipokwenda kushuhudia shughuli ya kunasua miili iliyobaki katika kivuko
hicho.
Amesema tume hiyo itaanza kazi mara moja na itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja.
Aidha,
Waziri Mkuu amewataja baadhi ya wajumbe watakaokuwa katika tume hiyo
ambao ni Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi, aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa
Temesa, Mhandisi Celina Magessa na Wakili Julius kalolo ambaye atasaidia
mapitio ya sheria na mfumo mzima wa uendeshaji wa vivuko.
“Lakini
yumo pia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi kwa ajili ya kusimamia stahili
na kina mama, aliyekuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius
Wambura, Bashiru Hussein kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
maafa .Wajumbe hao wanaanza kazi mara moja, waje niwape hadidu za
rejea,” amesema Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment