Bodi
 ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa KCB Bank Group, 
wameungana na waombolezaji wa msiba uliotokana na kuzama kwa kivuko cha 
MV Nyerere kwa kuchangia kiasi cha fedha taslim shilingi 125,000,000/=
Akikabidhi
 msaada huo wa fedha Mkurugenzi wa Bodi ya KCB, Zuhura Muro, alieleza 
kuwa wameguswa na maafa hayo na hivyo wanaahidi kuungana na serikali 
kadri wanavyoweza.
"Tunajua
 hatuwezi kumaliza shida au mahitaji ya waathirika hawa, hivyo tunapenda
 kuhamasisha taasisi nyingine zinazoguswa  kama sisi kutoa misaada yao 
ya hali na mali, huku tukiwaombea marehemu wapumzike  kwa amani na 
majeruhi majeruhi wapate kupona haraka," amesema.
Kutokana
 na kiasi hicho kilichotolewa na Bank KCB pamoja na michango ambayo  
wananchi na tasisisi mbalimbali zilizoguswa na kuchangia rambirambi 
katika maafa hayo imefikia jumla ya shilingi milioni 557






No comments:
Post a Comment