Mkazi
 wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika 
Mahakama ya Wilaya Kinondoni,   Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka 
matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akisomewa
 mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, 
Neema Moshi, alidai Julai 6  katika eneo la Hoteli ya White Sands  Mbezi
 Africana   Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina 
limehifadhiwa).
Shitaka la pili ni kuwa  kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu   Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.
Katika
 shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka 
huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa   CAG.






No comments:
Post a Comment