Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha masomo na udahili wa wanafunzi
wapya kwa ngazi zote za masomo na katika programu kwenye baadhi ya vyuo
vikuu kutokana na kukosa vigezo.
Pia imefuta vituo viwili vya vyuo vikuu na kuamuru wanafunzi wanaoendelea na masomo wahamishwe.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 25,
Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amevitaja vyuo hivyo
kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini (KIUT),
Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu kishiriki cha Marian
(MARUco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa
(CARUMUCo).
Vyuo
vingine ni Chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), Chuo kikuu
cha Mt. Yohana cha Tanzania (SJUT-St. Marks Centers na Chuo kikuu cha
Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).
Vyuo
hivyo ni pamoja na Chuo kikuu Teofilo Kisanji, Kituo cha Tabora na
Chuo kikuu Mt. Yohana cha Tanzania, Msalato (SJUT -Msalato Center).
Aidha,
amevitaja vyuo vilivyositishiwa utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi
wote wanaoendelea na masomo wahamishwe kuwa ni Mlima Meru (MMU), Chuo
Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo cha Eckernforde Tanga (ETU) cha Kilimo na
Teknolojia cha Jomo Kenyatta Kituo cha Arusha na Chuo Kikuu Kishiriki
cha Josiah kibira (JOKUCo).
“Asitokee
mwanafunzi yeyote akasajiliwa katika vyuo hivyo na wanaotakiwa kuhama
wawasiliane na vyuo vyao haraka,” amesema Profesa Kihampa.
Kwa
upande wake mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo (HELSB), Deus Changala
amesema waliokuwa na mikopo wasiwe na wasiwasi itapelekwa watakapokuwa.
No comments:
Post a Comment