Jukwaa
la Katiba Tanzania (Jukata) limelitaka Jeshi la Polisi na tume ya taifa
ya Uchaguzi (NEC) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na si kutumika
kisiasa.
Kauli
hiyo imetolewa jana Jumatano Septemba 19, 2018 na Mwenyekiti wa Jukata,
Hebron Mwakagenda katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo
amezungumzia hali ilivyokuwa katika uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la
Ukonga na Monduli pamoja na ule wa Udiwani katika kata 24.
Katika
ufafanuzi wake Mwakagenda amesema amesikitishwa na kitendo cha baadhi
ya polisi kushangilia uchaguzi kumalizika salama wakati waliotakiwa
kufanya hivyo ni wananchi.
"Polisi
wanashangilia hadharani bila aibu kuwa uchaguzi umefanyika kwa amani
kwani nani alitakiwa kuhakikisha kwamba amani hiyo inakuwepo si wao,
wanashangilia ushindi upi wakati ni wajibu wao kulinda mali raia na mali
zao”, alisema Mwakagenda.
Akiwazungumzia
NEC, Mwakagenda alisema tume hiyo haipaswi kupendelea upande wowote wa
chama cha siasa ili kuepuka kasoro ambazo hujitokeza katika chaguzi
mbalimbali ikiwemo za marudio, "Uchaguzi ni kama mechi, tume ndio refa
kwa hiyo kama itapendelea upande mmoja mechi haiwezi kuwa ya amani”.
Uchaguzi
huo umefanyika Septemba 16, 2018 ambapo baada ya matokeo kutangazwa ,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam walipongezana hadharani kwa kulinda amani kabla na baada
ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Ukonga, jambo ambalo katibu wa Itikadi na
Uenezi CCM, Humphrey Polepole alilipinga.
No comments:
Post a Comment