Mitambo
 na vifaa maalum vya kunyanyua, kubeba na kuvuta vitu vizito imewasili 
katika gati ya Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe tayari kufanya 
kazi ya kunyanyua na kugeuza kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka katika
 ziwa Victoria.
Mpaka
 kufikia jana wataalam wa uokoaji na masuala ya majini walifanikiwa 
kukilaza ubavu kivuko hicho ambacho awali kililala kifudifudi tangu 
kilipopinduka Septemba 20.
Mitambo
 na vifaa hivyo vimewasili asubuhi ya leo vikiwa ndani ya meli mbili 
kubwa binafsi za Mv Nyakibaria ya kampuni ya Mkombozi and Fisheries na 
Mv Orion II inayomilikiwa na kampuni ya Kamanga Ferry, zote za jijini 
Mwanza.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jana jioni, Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mv 
Nyerere, Isaac Kamwelwe alisema mitambo na vifaa hivyo vitarahisisha 
kazi ya kunyanyua, kugeuza na kukivutia ufukweni kivuko hicho.






No comments:
Post a Comment