Waziri
wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemani Jafo amewaagiza maofi sa wa elimu wa mikoa na
wilaya kuzingatia maadili kwa kuepuka vitendo vya upendeleo na
unyanyasaji wa walimu na wanafunzi.
Pia
amewataka kujiepusha na suala la uvujishaji mitihani, rushwa na utovu
wa maadili. Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri Joseph Kakunda
wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili kilichowakutanisha maofisa
elimu wa mikoa na halmashauri kilichofanyika jijini hapa, Jafo
alihimiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kusisitiza kuwa siku za hivi
karibuni, sekta hiyo imejijengea picha mbaya kwa mambo kadhaa.
“Tunatakiwa
kuepuka vitendo vya upendeleo na unyanyasaji wa aina yoyote kwa walimu
na wanafunzi, uvujaji wa mitihani, rushwa na utovu wa maadili kwa sababu
ninyi ni kioo cha jamii,” alisema.
Jafo
alionya kuwa vitendo vya utovu wa maadili kamwe havitavumiliwa na
serikali na yeyote anayeendekeza vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali.
“Nitumie fursa hii kulaani vitendo vya unyanyasaji na ukatili vilivyofanywa na baadhi walimu katika Shule ya Msingi Kibeta.”
Aidha, Jafo aliwaasa viongozi hao kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika utoaji wa adhabu kwa wanafunzi kote nchini.
Alitumia
nafasi hiyo kutoa msisitizo kwa viongozi hao kuwajibika kwa kufanya
kazi kwa bidii, weledi na kuitumikia umma, watumishi, wadau na marafiki
wa elimu ili kuendeleza imani iliyojengwa kwa umma.
Mkutano
huo umewakutanisha watendaji wa elimu katika ngazi ya taifa, mikoa na
halmashauri kwa lengo la kukumbushana majukumu, kujipima na kujitafakari
utendaji, kupeana uzoefu, kujenga uwezo na kujadiliana juu ya mbinu na
mikakati itakayotumika kusaidia kuboresha utoaji wa elimu bora.
No comments:
Post a Comment