Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi
mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia
ya kunyanyasana wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.
Lugola
pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa
kufanikisha mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya
kazi kwa kutegemeana.
Akizungumza
na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa
Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho
alikiitisha kwa lengo la kujuana na watumishi hao pamoja na kujua
changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.
“Mambo
muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya
kazi kwa bidii, kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika
tutapendana na kuzidi kufanikiwa,” alisema Lugola.
Lugola
aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa
haki zake au kucheleweshewa pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo
malipo mbalimbali ya watumishi wanayodai, na endapo yatatokea hayo
watumishi hao wamletee kero zinazowakabili ofisini kwake na kwa
kushirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyo watazitatua.
“Utumishi
wa umma naujua, na pia nimepitia manyanyaso kadhaa mpaka leo nimefikia
hapa kutokana na historia yangu, kwanini tusipendane?, kwanini
tunyanyasane?, kwanini tusishirikiane?, ni tabia mbaya na inatakiwa
kulaaniwa kwa baadhi ya wakuu wa idara na vitengo pamoja na wengineo
ambao wanatabia ya kunyanyasa watumishi waliochini yao,” alisema Lugola.
Mkutano
huo ambao ni wa kwanza kwa Waziri Lugola, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Meja Jenerali, Jacob Kingu pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan
Kailima, kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo tangu walipoteuliwa
miezi kadhaa iliyopita, walitaka kujuana zaidi na watumishi wa wizara
hiyo pamoja na kujua changamoto zao zinazowakabili. Toggle screen reader
support
Credit:
Felix Mwagara
Felix Mwagara
No comments:
Post a Comment