Zoezi
la ukoaji wa miili ya watu waliopoteza maisha katika Kivuko cha MV
Nyerere limeanza rasmi baada ya kusimama jana usiku, ambapo Vikosi
Maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa
Watanzania (JWTZ) na Jeshi la Zimamoto na uokoaji vinaendesha zoezi
hilo.
Hadi
sasa idadi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo
iliyotokea jana tarehe 20 Septemba 2018 imeongezeka kutoka watu 44 hadi
86.
Kivuko cha MV Nyerere kilizama katika Ziwa Victori kikitokea Bugorora kisiwani Ukerewe kuelekea Kisiwa cha Ukara.
Inahofiwa
kuwa, mamia ya watu waliokuwamo katika kivuko hicho wamepoteza maisha,
ambapo watu 37 walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai hapo jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Maghembe amesema kuwa sababu ya kuzama kwa
kivuko hicho inasadikika kuwa ilibeba watu zaidi ya 400 ambapo
kilizidisha uwezo wake ambao ni watu 101.
Maghembe amesema kuwa imezama mita chache kabla ya kuwasili eneo la Ukara ambapo dereva alipunguza mwendo kuashiria amekaribia kutia nanga ndipo abiria wengi walihamia upande wa lango la kutokea wakiwahi kusogea ili washuke ndipo uzito ulizidi na kupinduka.
“Abiria walipoona mwendo umepunguzwa walikimbilia kuwahi mbele ya lango ili kujiandaa kushuka, ndipo uzito ukaegemea upande mmoja”, amesema Maghembe

No comments:
Post a Comment