Imeelezwa
kuwa sehemu pekee ya kuimarisha kilimo cha mwananchi mmoja mmoja,
wananchi katika makundi ya kijamii hususani vijana ni kupitia sekta ya
kilimo kwani ndio sehemu pekee ya ukombozi wa mkulima katika jamii.
Imeelezwa
kuwa kuna uwezekano wa kufanya biashara mbalimbali nchini ambazo
zinaweza kuongeza kipato lakini sahemu sahihi isiyokuwa na jazba na
dhoruba katika utendaji ni kufanya kilimo biashara ambacho kamwe
hakiwezi kumtupa mkulima.
Dkt
Charles Tizeba Waziri wa kilimo, ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba
2018 wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Vijana
hao ambao wameamua kutumia nguvu zao pasina malipo wameamua kwa umoja
wao kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa
kauli yake inayohamasisha chachu na juhudi za kiutendaji kwa wananchi ya
“Hapa Kazi Tu”.
Aidha,
katika kuhamasisha juhudi za kiutendaji Waziri huyo mwenye dhamana ya
kilimo ameunga mkono juhudi za vijana hao kwa kuchangia fedha ya chakula
shilingi 1,100,000 sambamba na kushiriki ujenzi wa jengo maalumu la
upasuaji.
Waziri
wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alitembelea ujenzi huo wa Hospitali ya
Wilaya ya Muheza akiwa safarini kutembelea mashamba ya mkonge ikiwa ni
siku ya pili ya ziara ya kikazi Mkoani Tanga aliyoianza jana tarehe 25
Septemba 2018 ya kukutana na makundi mbalimbali ya wakulima wa zao la
Mkonge ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima wa
zao hilo.
No comments:
Post a Comment