Benki Kuu ya Tanzania imewataka wananchi kuheshimu fedha ya Tanzania kwani ni moja ya alama ya taifa.
Kauli
hiyo imekuja kufuatia matukio ya hivi karibuni ya baadhi ya wananchi
kutoziheshimu, kuzifanyia dhihaka na kebehi noti za Jamhuri ya Mungano
wa Tanzania.
Taarifa
ya BoT kwa vyombo vya habarI ambayo inasema utunzaji mzuri wa fedha
zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza
gharama za uchapishaji.
"Kwa
mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha
26, BoT ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," imesema taarifa hiyo.
Pia
imesema noti na sarafu hizo zina alama muhimu inayolitambulisha taifa
la Tanzania ambayo ni nembo ya Bwana na Bibi. Imefafanua alama hiyo
inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwa mfano Bendera ya
Taifa.
Pia
noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal
tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika na pia Benki Kuu
pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu.
Taarifa
hiyo imefafanua kuhusu hilo kupitia kifungu cha 28 kikisomwa pamoja na
kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.
"Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.
"Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.
No comments:
Post a Comment