Vyama vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.
Hayo
 yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji Francis 
Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa vyama
 vya siasa jana  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea vyama 
uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze 
kujiendesha kama taasisi.
Jaji
 Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga vyama kama 
taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika 
vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati 
chafu kutoka Ofisi yaMdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
‘’Mafunzo
 ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile mali za vyama ni muhimu
 kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni vyema mkatambua kuwa
 vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji wa ndio maana 
msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji Mtungi.
Aidha
 Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa elimu ya 
fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili linasaidia 
sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.
Wakati
 huo huo Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa 
Rwekaza Mkandala ambaye aliwasilisha mada ya Jinsi ya Kuendesha chama 
kama taasisi,alisema lengo la chama cha siasa chochote ni kujiandaa 
kushika madaraka au kuwa wapinzani wa serikali hivyo lazima kuhakikisha 
vinajijenga kama taasisi inayoaminika kwa wananchi.
Profesa
 Mkandala alisema siasa vyama vingi hapa Nchini ni matokeo ya ukoloni 
mamboleo ambao ulianza kushamiri hapa nchini kwa miaka 1990 ambapo nchi 
ya Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Barani Afrika zilikumbwa na 
mabadiliko ya kiuchumi ya soko huria ikiwemo nchi zilizokuwa za ujamaa 
kuanza kufuata m asharti ya Shirika la Fedha Duniani IMF.
Aidha
 Profesa Mkandala alitaja vigezo vinavyofanya chama kuwa Taasisi muhimu 
kuwa ni Itikadi, Uongozi bora, Wanachama, Sera na programu za chama, 
Rasilimali






No comments:
Post a Comment